Posts

Matukio katika picha Wataalam wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya na Mkoa wa Dodoma wakitoa elimu katika Mkutano wa Maaskofu 600 wa TAG Tanzania Bara na Visiwani

Image
 

Madiwani wa Jiji la Dodoma katika Mkutano wa Baraza la Madiwani

Image
 

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Joseph Fungo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani

Image
 

Muonekano wa Madiwani katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Jiji la Dodoma

Image
 

Prof. Davis mwamfupe katika mkutano wa Baraza la Madiwani

Image
 

JIJI LA Dodoma linajali wanafunzi

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inawaonea huruma na kuwajali wanafunzi kwa watengenezea mazingira mazuri ya kujifunzia. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alipokuwa akijibu swali la Diwani wa Hazina, Samwel Mziba aliyetaka kujua ni lini halmashauri itakuwa na huruma kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru kwa kuifanyia ukarabati mkubwa ili iendane na hadhi ya jiji. Fungo alisema kuwa halmashauri inawaonea huruma wanafunzi na kuwajali kwa wajengea miundombinu ili waweze kusoma katika mazingira bora na salama. “Mheshimiwa mwenyekiti, tulimpeleka mhandisi kufanya makadirio ya gharama za kufanya ukarabati wa madarasa yaliyochakaa katika shule hiyo na mipaka kwa ajili ya ujenzi wa uzio. Hadi sasa mbao na ‘gypsum board’ zimeshafika shuleni kwa ajili ya kufanya ukarabati wa shule hiyo” alisema Fungo. Aidha, Mstahiki Meya alisema kuwa kuna utayari ...

Mchakato kugawa mitaa kuanzia kwenye mitaa

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WANANCHI wametaarifiwa kuwa mchakato wa kugawa maeneo ya mitaa ambayo yanaonekana makubwa ili kusogeza huduma karibu na wananchi unaanzia katika ngazi ya mtaa. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo akijibu maswali ya papo kwa papo Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alipokuwa akijibu swali la papo kwa papo la Diwani wa Kata ya Iyumbu, Richard Sutuchi aliyetaka kujua utaratibu wa wa kugawa maeneo ya mitaa ili kusogeza huduma kwa wananchi katika Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Fungo, alisema kuwa utaratibu wa kugawa mitaa unaanzia katika mitaa husika. “Mapendekezo yanatoka katika mitaa husika na utaratibu huo unapelekwa katika kikao cha kamati ya maendeleo ya kata hadi halmashauri. Hivyo, mchakato uanzie kwenye mtaa” alisema Fungo. MWISHO

Dodoma Sec yateuliwa ufundishaji mubashara nchini

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma limetaarifiwa kuwa Shule ya Sekondari Dodoma imeteuliwa kuwa miongoni mwa shule 10 za majaribio ya ufundishaji mubashara nchini. Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Madiwani, Prof. Davis Mwamfupe akisisitiza jambo Taarifa hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Madiwani, Prof. Davis Mwamfupe alipokuwa akitoa taarifa ya Mwenyekiti katika Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Prof. Mwamfupe alisema kuwa Shule ya Sekondari Dodoma imeteuliwa kuwa miongoni mwa shule 10 za majaribio nchini ya ufundishaji mubashara kwa njia ya mtandao. Alisema kuwa ufundishaji huo unamuwezesha mwalimu wa shule moja kufundisha idadi kubwa ya shule kadri inavyowezesha. “Mwalimu yupo Shule ya Sekondari Kibaha anafundisha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dodoma na wanafunzi wote wanamuona na wanapata fursa ya kuuliza maswali na kujibiwa. Gharama ya mtambo...

Wazazi Chamwino washauriwa kutenga muda kuzungumza na watoto

Image
  Na. Dennis Gondwe, CHAMWINO WAZAZI na walezi katika Wilaya ya Dodoma wameshauriwa kutenga muda wa kukaa na kuongea na watoto wao ili waweze kubaini changamoto zinazowakabili ikiwemo kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia. Cpl. Edith Siwango kutoka Dawati la Jinsia na Watoto wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Dodoma alipokuwa akiongea na wanafunzi, walimu na wadau wa Lishe katika Shule ya Msingi Chamwino Ushauri huo ulitolewa na Cpl. Edith Siwango kutoka Dawati la Jinsia na Watoto wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Dodoma alipokuwa akiongea na wanafunzi, walimu na wadau wa masuala ya Lishe katika Shule ya Msingi Chamwino iliyopo Kata ya Chamwino Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Cpl. Siwango alisema “tupo hapa kwa ajili ya kuwalinda watoto wetu. Wazazi na walezi mlio hapa nawaomba mtenge muda wa kuzungumza na watoto wenu. Mazungumzo hayo yatawasaidia kuwaelewa watoto wenu. Watoto wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali zinazohusisha ukatili wa kijinsia na kushindwa kuwaeleza wazazi na ...

MAMIA WAJITOKEZA KUMUAGA LOWASA KARIMJEE, WAKO PIA VIONGOZI WA DINI

Image
  MAMIA ya watu wamejitokeza katika Viwanja vya Karimejee jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, huku zoezi hilo likitarajiwa kuongozwa na Makamu wa Rais, Dkt. Phillip Mpango. Leo Jumanne, Februari 12, 2024, mwili wa Lowassa unatarajiwa kuagwa katika Viwanja hivyo ambapo viongozi mbalimbali wa kiserikali akiwemo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mawaziri wengine wamehudhuria. Mbali na mawaziri wa Tanzania Bara, Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Othman Masoud Othman na mawaziri kadhaa wa visiwa hivyo, wamehudhuria kwa ajili ya kushiriki hafla hiyo ya mwisho kwa Lowasa. Viongozi wengine wa vyama vya siasa akiwemo Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na viongozi wa dini, wamehudhuria shughuli hiyo. Jeneza lililobeba mwili wa Lowassa huku likiwa limefunikwa na bendera ya Tanzania, limeingia uwanjani hapo majira ya 10.20. Shughuli hiyo inatanguliwa na ibada fupi inayoongozwa...