Mchakato kugawa mitaa kuanzia kwenye mitaa
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
WANANCHI
wametaarifiwa kuwa mchakato wa kugawa maeneo ya mitaa ambayo yanaonekana
makubwa ili kusogeza huduma karibu na wananchi unaanzia katika ngazi ya mtaa.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo akijibu maswali ya papo kwa papo |
Kauli
hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo
alipokuwa akijibu swali la papo kwa papo la Diwani wa Kata ya Iyumbu, Richard
Sutuchi aliyetaka kujua utaratibu wa wa kugawa maeneo ya mitaa ili kusogeza
huduma kwa wananchi katika Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Fungo,
alisema kuwa utaratibu wa kugawa mitaa unaanzia katika mitaa husika.
“Mapendekezo yanatoka katika mitaa husika na utaratibu huo unapelekwa katika
kikao cha kamati ya maendeleo ya kata hadi halmashauri. Hivyo, mchakato uanzie
kwenye mtaa” alisema Fungo.
MWISHO
Comments
Post a Comment