Dodoma Sec yateuliwa ufundishaji mubashara nchini
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
BARAZA
la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma limetaarifiwa kuwa Shule ya Sekondari
Dodoma imeteuliwa kuwa miongoni mwa shule 10 za majaribio ya ufundishaji
mubashara nchini.
Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Madiwani, Prof. Davis Mwamfupe akisisitiza jambo |
Taarifa
hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Madiwani, Prof. Davis Mwamfupe
alipokuwa akitoa taarifa ya Mwenyekiti katika Mkutano wa Baraza la Madiwani
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Prof.
Mwamfupe alisema kuwa Shule ya Sekondari Dodoma imeteuliwa kuwa miongoni mwa
shule 10 za majaribio nchini ya ufundishaji mubashara kwa njia ya mtandao.
Alisema kuwa ufundishaji huo unamuwezesha mwalimu wa shule moja kufundisha
idadi kubwa ya shule kadri inavyowezesha.
“Mwalimu
yupo Shule ya Sekondari Kibaha anafundisha wanafunzi wa Shule ya Sekondari
Dodoma na wanafunzi wote wanamuona na wanapata fursa ya kuuliza maswali na
kujibiwa. Gharama ya mtambo mmoja wa kusimika mfumo huu ni shilingi 67,000,000
kwa shule ya Dodoma sekondari. Hivyo, tutaangalia jinsi ya kuwezesha shule za
pembezoni mwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuweza kuwa na mfumo huo” alisema
Prof. Mwamfupe.
MWISHO
Comments
Post a Comment