JIJI LA Dodoma linajali wanafunzi
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
HALMASHAURI
ya Jiji la Dodoma inawaonea huruma na kuwajali wanafunzi kwa watengenezea
mazingira mazuri ya kujifunzia.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo |
Kauli
hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo
alipokuwa akijibu swali la Diwani wa Hazina, Samwel Mziba aliyetaka kujua ni
lini halmashauri itakuwa na huruma kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru kwa
kuifanyia ukarabati mkubwa ili iendane na hadhi ya jiji.
Fungo
alisema kuwa halmashauri inawaonea huruma wanafunzi na kuwajali kwa wajengea
miundombinu ili waweze kusoma katika mazingira bora na salama. “Mheshimiwa
mwenyekiti, tulimpeleka mhandisi kufanya makadirio ya gharama za kufanya
ukarabati wa madarasa yaliyochakaa katika shule hiyo na mipaka kwa ajili ya
ujenzi wa uzio. Hadi sasa mbao na ‘gypsum board’ zimeshafika shuleni kwa ajili
ya kufanya ukarabati wa shule hiyo” alisema Fungo.
Aidha,
Mstahiki Meya alisema kuwa kuna utayari wa baadhi ya wananchi waliosoma katika
shule ile kuchangia ukarabati huo wanasubiri hatua za awali zianze.
MWISHO
Comments
Post a Comment