Umeme wa REA chachu ya viwanda vidogo vidogo Kata ya Ipala
Na. John Masanja, IPALA Awamu ya kwanza ya umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umechochea shughuli za maendeleo na kuinua uchumi wa wananchi katika Kata ya Ipala, Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Kata ya Ipala, George Magawa wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofanya ‘media tour’ kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali katika kata hiyo kuanzia mwaka 2021 hadi 2025. Alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imepeleka huduma ya umeme katika Kata ya Ipala. “Kata yetu imefikiwa na awamu ya kwanza ambayo ina faida nyingi sana. Wananchi wanafanya shughuli mbalimbali zinazojumuisha matumizi ya umeme kwa kiwango kikubwa na naamini kwa siku za usoni hapa kwetu kutakuwa mtaa wa viwanda vya aina tofauti” alisema Magawa. Nae mkazi wa Kata ya Ipala, Mathias Masita aliishukuru serikali kwa kuwapelekea umeme kwasababu maisha yao yamebadilika na wanafanya shughuli zinazohusisha umeme kwa kiwango kikubwa. “Mradi wa REA umetunufaisha s...
Comments
Post a Comment