Osterbay Dodoma wajitokeza usafi wa mazingira
Na.
Dennis Gondwe, KIWANJA CHA NDEGE
WANANCHI
wa Mtaa wa Osterbay, Kata ya Kiwanja cha Ndege Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamejitokeza
kufanya usafi wa mazingira katika eneo la Shule ya Msingi Mlimwa B kwa lengo la
kuweka mazingira safi na kuepuka na magonjwa ya mlipuko kwa wanafunzi na jamii
kwa ujumla.
Kauli
hiyo ilitolewa na Afisa Mtendaji Mtaa wa Osterbay, Ashura Iberia alipokuwa
akiongea na wananchi wa Mtaa wa Osterbay waliojitokeza kwa wingi kufanya usafi
wa mazingira katika Shule ya Msingi Mlimwa B.
Iberia
alisema “leo tumefanya usafi wa mazingira kuzunguka Shule ya Msingi Mlimwa B,
wananchi wa Mtaa wa Osterbay wamejitokeza kwa wingi kufanya usafi wa mazingira.
Lengo la kufanya usafi huo ni kuweka mazingira ya shule safi ili wanafunzi
ambao ni watoto wetu wasome katika mazingira safi na salama. Lakini pia
kuwaepusha wanafunzi na jamii inayozunguka shule hii na magonjwa ya mlipuko.
Zoezi hili nimelisimamia mimi mwenyewe Afisa Mtendaji Mtaa wa Osterbay ili
kutoa chachu na hamasa kwa usafi wa mazingira kwa kila mwananchi”.
Kwa
upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Mtaa wa Osterbay, Hussein Ngura alisema kuwa kuanzia
siku hiyo usafi ni agenda ya mtaa. “Kuanzia leo agenda yetu kuu ya Mtaa wa Ostebay
ni usafi wa mazingira kama alivyosema Afisa Mtendaji wa Mtaa. Kama tutakumbuka
aliwahi kufika hapa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma na kukagua usafi kwa kustukiza. Sasa
hatujui ni kiongozi gani atafuata kuja kukagua, hivyo lazima tujipange kwa
kuweka mazingira yetu safi. Wananchi wa Mtaa wa Osterbay mmenitendea imani kuwa
nina watu kwa jinsi mlivyojitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hili la usafi wa
mazingira. Pia, mimi namsifu sana Afisa Mtendaji wa Mtaa wetu kwa kazi nzuri anayofanya,
hakika ni mchapa kazi hodari na anatuongoza vizuri” alisema Ngura.
Zoezi
la usafi wa mazingira katika Mtaa wa Osterbay, Kata ya Kiwanja cha Ndege
liliongozwa na Afisa Mtendaji wa Mtaa, na kuhudhuriwa na wenyeviti, mabalozi na
mamia ya wananchi.
MWISHO
Comments
Post a Comment