Usafi wa Mazingira Kipaumbele Kata ya Chamwino
Na. Dennis Gondwe, CHAMWINO
CLUB
ya Mazingira ya Shule ya Sekondari Hijra imeshiriki zoezi la usafi wa mazingira
pembezoni mwa barabara inayoelekea katika makaburi ya Hijra urefu wa takribani mita 200
kwa kufyeka majani, kuokota taka ngumu na makopo ili kuweka viunga vya barabara
hiyo safi.
Akitoa
shukrani baada ya zoezi hilo, Afisa Mtendaji Kata ya Chamwino, Lucas Mkelege
alisema kuwa uongozi wa Shule ya Sekondari Hijra umeonesha mfano mzuri kupitia
Club yake ya Mazingira. “Mtakumbuka kuwa tangu kuanzishwa kwa Club ya Mazingira
katika Shule ya Sekondari Hijra mwaka 2023 imekuwa mstari wa mbele katika suala
ya usafi wa mazingira. Nakumbuka malengo ya club hiyo pamoja na mambo mengine
ni kuwajengea wanafunzi moyo wa uzalendo na kushiriki masuala ya kijamii
ikiwemo kudumisha usafi wa mazingira, asanteni sana” alishukuru Mkelege.
Kata
ya Chamwino imekuwa mstari wa mbele katika masuala ya usafi wa mazingira ikiwa
na muitikio mkubwa wa wananchi kushiriki usafi wa pamoja wa mazingira.
MWISHO
Comments
Post a Comment