CCM CHANG’OMBE YAPONGEZA MPANGO WA ULINZI KATIKA MITAA
Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chang’ombe kimepongeza mipango ya ulinzi na usalama
katika mitaa ya kata hiyo na kuitaja kuwa ni mizuri.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Chang’ombe, Bashir Iddy |
Kauli
hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Chang’ombe, Bashir Iddy alipokuwa
akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Ofisi ya
Serikali ya Mtaa wa Hamvu jijini Dodoma.
Iddy
alisema “mipango yenu kwenye ulinzi na usalama ndani ya mitaa ni mizuri. Lakini
pia, mipango yenu ya kuishi na wananchi ndani ya mitaa nayo ni mizuri.
Wenyeviti wa mitaa nawashukuru sana kwa hilo. Vilevile, nawashukuru watendaji
wetu ngazi ya kata, Mtendaji wa Kata, Afisa Maendeleo ya Jamii Kata, Afisa
Ustawi wa Jamii Kata, Mratibu wa Elimu Kata, Afisa Afya Kata na wataalamu wote
mnafanya kazi nzuri, kwa sababu leo Kata ya Chang’ombe ina sifa, mmeboresha
mifumo ya vikundi vya ujasiriamali. Kila mtaa tumepita kuna vikundi
vinavyopokea mikopo ndani ya Halmashauri yetu. Hizi ni kazi nzuri zinazoongozwa
na Ofisi ya Mtendaji wa Kata”.
Mwenyekiti
huyo alipongeza taatifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika mitaa.
“Nawashukuru sana watendaji wote wa mitaa kwa kuandaa taarifa zenu nzuri zenye
tija ambayo inatuonesha mipango yenu yote mnayoifanya katika mitaa yenu. Na hii
ndiyo sifa kubwa ya CCM kujivunia elimu bora, siasa safi inayoendeshwa katika
vyuo vyetu. Hali kadhalika, kupata wataalamu wazuri ambao wanakuja kusimamia
ndani ya mitaa yetu” alisema Iddy.
Mwananchi
Jasmin Abdallah alisema kuwa ana imani wa watedanji kutokana na kuwa wapya na
kusema kuwa watawasaidia katika kutatua changamoto zinazowakabili.
MWISHO
Comments
Post a Comment