DIWANI FUNDIKILA APONGEZWA UWEKEZAJI SOKO LA HAMVU
Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE
DIWANI
wa Kata ya Chang’ombe, Bakari Fundikila amepongezwa kwa jitihada zake za
kuwaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo ikiwa ni pamoja na uwekezaji katika Soko
la Hamvu.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chang’ombe, Bashir Iddy |
Pongezi
hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chang’ombe, Bashir
Iddy katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa
Hamvu jijini Dodoma.
Iddy
alisema “tunaendelea kumshukuru Diwani Bakari Fundikila kwa kufanya uwekezaji
mkubwa katika Soko la Hamvu, tayari ametufahamisha kuwa kiasi cha shilingi
20,000,000 zipo tayari katika akaunti ya kata kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo.
Jitihada zote hizo anazifanya kwa kushirikiana na Mheshimiwa Athony Mavunde
ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini. Huyu ndugu yetu Mbunge lazima
tumwangalie kwa macho yote mawili kwasababu amejitoa katika kada zote ikiwemo
elimu, michezo, afya na maendeleo. Sasa, maendeleo yote haya yatafanyika ikiwa
tutawaunga mkono. Ndugu zangu twendeni tukashirikiane. Chama Cha Mapinduzi
kinataka kukuza maendeleo katika maeneo yake, lakini sisi wananchi na wanachama
tuwe tayari kuunga mkono”.
Nasrat
Mussa mkazi wa Hamvi alisema kuwa ujenzi wa soko la Hamvu utaongeza wigo kwa
wananchi kufanya biashara zao sehemu rasmi tofauti na wanavyofanya sasa.
MWISHO
Comments
Post a Comment