CHANG’OMBE WAJIVUNIA UJENZI KITUO CHA POLISI
Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE
WANANCHI
wa Kata ya Chang’ombe wanajivunia mradi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi katika
kata yao jambo litakaloondoa uhalifu na kuwahakikishia usalama wao na mali zao.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chang’ombe, Bashir Iddy |
Kauli
hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chang’ombe, Bashir
Iddy alipokuwa akiongea na wanachama wa CCM na wananchi wa Kata ya Chang’ombe
katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Hamvu jijini Dodoma.
Iddy
alisema kuwa Diwani wa Kata ya Chang’ombe, amekuwa akiipambania kata hiyo
katika miradi mbalimbali ya maendeleo. “Ndugu wanachama wa CCM na wananchi,
Diwani wenu Bakari Fundikila amekwenda kusimamia mradi wa ujenzi wa Kituo cha
Polisi Chang’ombe. Kituo kile takwimu zinaonesha baada ya Makao Makuu ya Polisi
Wilayaya Dodoma, kinachofuata ni kituo hiki cha Polisi Chang’ombe. Na
tumemsikia Diwani hapa amesema kituo hiki mmekijenga wanachama wa CCM na
wananchi wa Chang’ombe kwa nguvu zenu wenyewe. Mheshimiwa Diwani tunazidi
kukupongeza kwa kazi nzuri” alisema Iddy.
Kijana
Issa Mwenda mkazi wa Changombe alisema kuwa ujenzi wa Kituo cha Polisi
Chang’ombe utaongeza hali ya usalama kwa wakazi na mali zao.
MWISHO
Comments
Post a Comment