USALAMA MTAA WA MAZENGO NI SHWARI
Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE
HALI ya ulinzi na usalama katika Mtaa wa Mazengo ni
shwari na wananchi wanaendelea kutekeleza shughuli za maendeleo.
Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mazengo, Godfrey Nkinda akisoma taarifa ya Mtaa |
Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mazengo,
Godfrey Nkinda alipowasilosha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Mazengo.
Nkinda alisema kuwa hali ya ulinzi na usalama katika Mtaa
wa Mazengo uliyopo Kata ya Chang’ombe ni shwari. “Uongozi wa serikali ya Mtaa
wa Mazengo umekuwa ukishirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha mtaa unakuwa
salama. Polisi wamekuwa wakikabiliana na matukio madogomadogo ambayo ni
viashiria vya uhalifu. Jeshi la Polisi kupitia Polisi kata na jamii wamekuwa
wakifanya doria na misako ili kubaini maeneo chochezi ambayo ni vijiwe vya
kuvutia bangi hasa maeneo ya Mapagale jambo ambalo Polisi wamefanikiwa
kulipunguza na kazi ya kukabiliana na hali hiyo bado inaendelea” alisema
Nkinda.
Alisema kuwa vikao vya ulinzi na usalama vimekuwa
vikifanyika kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mtaa kwa kushirikiana na
wenyeviti wa mashina ili kuendelea kupeana taarifa juu ya uwepo wa viashiria
vya uhalifu.
Kwa upande wake mwananchi wa mtaa huo John Vene alisema
kuwa suala la ulinzi na usalama nilawahusu wananchi moja kwa moja. “Hatuwezi
kuwategemea Polisi kwa sababu wapo wachache pamoja na kuwa na mafunzo ya
kukabiliana na uhalifu” alisema Vene.
MWISHO
Comments
Post a Comment