Posts

HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA YAPATA HATI SAFI YA UKAGUZI WA HESABU

 

Waziri Mkuu Mgeni Rasmi NBC Dodoma Marathon 2023

Image
  Dodoma, Julai 19, 2023 – Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika mbio za NBC Dodoma Marathon 2023 zinazotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili tarehe 23 Julai 2023. Mbio za mwaka huu zinalenga kukusanya jumla ya shilingi milioni 500. Fedha hizo zitatumika kusaidia kupambana na kansa ya shingo ya kizazi pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa wakunga ikiwa ni sehemu ya kusaidia kuongeza wataalamu ili kupunguza vifo vya uzazi. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma kuhusu maandalizi ya mbio hizo zilizojizolea umaarufu mkubwa na ambazo zinafanyika kwa mara ya nne mfululizo mwaka huu, mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule alisema mkoa umejipanga vyema kuwapokea wakiambiaji na wageni wote wataoshiriki. “Kwanza kabisa napenda kuishukuru benki ya NBC kwa kuandaa mbio hizi zenye faida kubwa kwetu kama nchi. Pili niwahakikishie washiriki wote kuwa sisi kama mkoa wa Dodoma tumejipanga vy...

WAAJIRIWA SEKTA BINAFSI WATAKIWA KUZINGATIA KIMA KIPYA CHA MSHAHARA

Image
Na. Mwandishi Wetu,  Dodoma OFISI ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Idara ya Kazi imewataka waajiri wa sekta binafsi nchini kuzingatia kima kipya cha chini cha mshahara kilichotangazwa na serikali mwaka huu kwa kuwa ni takwa la kisheria. Kamishna wa Kazi Msaidizi  anayeshughulikia  Mahusiano kazini  Bw.  Andrew Mwalwisi akitoa elimu kwa umma jijini Dodoma kuhusu sheria na miongozo ya kazi   Kima hicho kilitangazwa katika kupitia tangazo la serikali namba 687 na kilianza kutumia Januari mosi, 2023 na kimewekwa kwenye sekta kuu 13. Kamishna wa Kazi Msaidizi, Mahusiano kazini wa Ofisi hiyo, Andrew Mwalwisi ameyasema hayo Julai 19, 2023 alipokuwa akitoa elimu kwa umma jijini Dodoma kuhusu sheria na miongozo ya kazi. Amesema kwa sekta ya kilimo ni Sh.140,000, afya (Sh.195,000), mawasiliano imegawanyika kuna sekta ya huduma za mawasiliano (Sh.500,000), huduma za utangazaji na vyombo vya habari, posta usafirishaji vifurushi ...

KAMATI YA FEDHA JIJI LA DODOMA YATEMBELEA KIKUNDI CHA NASHA

Image
 

Naibu Waziri Nderiananga ateta na Wanafunzi wa Weruweru

Image
Na. Mwandishi Wetu- Moshi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga awaasa vijana kujikinga na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ili kuyafikia malengo waliyonayo. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Ummy Nderiananga akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Weruweru alipowatembelea shule hiyo Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Weruweru alipotembelea mapema Julai 16, 2023 shuleni hapo kwa lengo la kuwapa hamasa wanafunzi wa shule hiyo ambayo aliwahi kusoma na kutoa zawadi za taulo za kike na mafuta ya ngozi kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa uongozi wa shule hiyo. Mhe. Nderiananga aliwaeleza upo umuhimu wa kuendelea kuchukua tahadhari za masuala yanayohusu Virusi vya UKIMWI kwani kwa mujibu wa tafiti za viashiria vya VVU na UKIMIWI mwaka 2016/17 zinaonesha kuwa asilimia kubwa ya maambukizi ipo kwa vijana mweny...

CLUB YA MAZINGIRA YA SHULE YA SEKONDARI HIJRA KATA YA CHAMWINO ILIVYOSHIRIKI ZOEZI LA USAFI WA MAZINGIRA SIKU YA JUMAMOSI

Image
 

MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR AWATAKA WAFANYAKAZI KUIGA TABIA NJEMA ZA WASTAAFU

Image
  Na Faki Mjaka-AGC Zanzibar Mwanasheria wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji amewataka Wafanyakazi kuiga tabia njema za Wafanyakazi wastaafu ikiwemo kutunza siri za Ofisi ili kujiweka salama wao na Ofisi wanazozifanyia kazi. Dkt. Mwinyi aliyasema hayo katika hafla ya kumuaga aliyekuwa Katibu Muhtasi wa Ofisi hiyo ambaye amestaafu Bi Masunya Juma Abdalla huko katika ukumbi wa Ofisi hiyo Mazizini mjini Unguja. Alisema ni jukumu la kila mmoja kuchukua yale mema ambayo wafanyakazi walijifunza kutoka kwake ikiwemo kufanya kazi kwa bidii, nidhamu na ustahamilivu. Dkt. Mwinyi alisema Bi Masunya alitanguliza uzalendo na maslahi makubwa ya nchi kwa kuamini kuwa Taasisi anayofanyia kazi ni muhimu ambayo inahitaji mtu mwenye bidii ya kazi jambo lililomjengea sifa ya kuwahi kazini na kuchelewa kutoka siku zote. Aliwataka wafanyakazi hao kila mmoja kuweka nia na mikakati ya kuhakikisha anaagwa kwa wema kutokana na utumishi wake uliotukuka kama ilivyofanyika kwa Bi Masu. “Kukusanyika hapa tukafur...

RAIS DKT.MWINYI ASHUHUDIA UTIAJI WA SAINI YA MKOPO WA FEDHA KWA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KUTOKA KWA MABENKI YA NMB NA NBC

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akishuhudia utiaji wa Saini wa Fedha za Mkopo kutoka kwa Benki ya NBC kwa kushirikiana na Benki ya NMB, kwa upande wa Benki ya NBC akisaini Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Ndg.Theobald Sabi  (kulia kwa Rais) na kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akisaini Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Dkt.Juma Malik Akili (kushoto kwa Rais) hafla hiyo ya utiaji wa saini iliyofanyika leo 14-7-2023 katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. (Picha na Ikulu) BAADHI ya Viongozi wa Serikali na wa Benki ya NMB na NBC wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi akihutubia wakati wa utiaji wa saini wa Fedha za Mkopo zinazotolewa kwa kushirikiana na benki hizo kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 14-7-2023.(Picha na Ikulu)  

Kauli ya RC Senyamule kuhusu Hati ya Ukaguzi wa Hesabu Jiji la Dodoma

Image
 

Kauli ya DC Shekimweri kuhusu hoja za ukaguzi Jiji la Dodoma

Image