Na. Dennis Gondwe, DODOMA DIWANI wa Viti Maalum, Joan Mazanda aliibuka kidedea kwa kupata kura 15 na kuongoza Kamati ya kudumu ya Uchumi, Elimu na Afya katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Uchumi, Elimu na Afya, Joan Mazanda Akitangaza matokeo hayo, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Alimwoni Chaula alisema kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ya Uchumi, Elimu na Afya ni Joan Mazanda. “Kamati ya kudumu ya Uchumi, Elimu na Afya ilikuwa na wagombea watatu wa nafasi ya mwenyekiti. Matokeo yalikuwa ni kama ifuatavyo. Mheshimiwa Andrew Muholo, Diwani wa Ipala alipata kura tatu; Mheshimiwa Fatuma Zollo, Diwani wa Viti Maalum alipata kura nne na Mheshimiwa Joan Mazanda, Diwani wa Viti Maalum alipata kura 15. Hivyo, mshindi ni Mheshimiwa Joan Mazanda” alisema Chaula. Katika hatua nyingine, Diwani wa Kata ya Madukani, Prof. Davis Mwamfupe alitoa pongezi kwa Diwani Mazanda kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamat...
Comments
Post a Comment