Jiji la Dodoma kukusanya shilingi 1,902,895,000.00 kutoka Soko la wazi la Machinga
Na. Asteria Frank, DODOMA
Halmashauri
ya Jiji la Dodoma imepanga kukusanya kiasi cha shilingi 1,902,895,000.00 kutoka
vyanzo mbalimbali vya mapato katika Soko la wazi la Machinga ili kuweza kuboresha
utoaji wa huduma kwa wananchi katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa
fedha 2024/2025.
Kauli
hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko
wakati akisoma taarifa ya uendeshaji wa Soko la wazi la Machinga kwa Kamati kudumu
ya Bunge ya Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa iliyofanya ziara ya kutembelea
na kukagua maendeleo ya soko hilo lililopo eneo la Bahi Road jijini Dodoma.
Dkt.
Sagamiko alisema kuwa ujenzi wa soko hilo uligharimu kiasi cha shilingi
9,529,747,200.66. Kati ya fedha hizo shilingi 6,529,747,200.66 ni mapato ya
ndani ya Halmashauri ya Jiji, shilingi 2,500,000,000.00 ni ruzuku kutoka
Serikali kuu na shilingi 500,000,00.00 ni fedha za Mpango wa Maendeleo kwa
Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko -19 na kuwa soko limekamilika na
tayari linatumika.
“Kwa
mujibu wa usanifu soko linatarajiwa kubebea wafanyabiashara wadogo 3,034. Hata
hivyo, wakati wa utekelezaji soko limekuwa na uwezo wa kubeba wafanyabiashara
2,553 ambapo wamegawanywa katika zoni 10 ambazo ni A, AB, B, BC, C, D, DE, E,
EF na F. Kutokana na ongezeko la wafanyabiashara wadogo katika soko hili
ililazimika kutengwa kwa eneo la mbele
ya soko na pembezoni ili kuweza kubeba wafanyabiashara 100 mpaka 200 ambao hupanga
biashara zao katika eneo maalumu ndani ya soko nyakati za jioni na hupaswa
kuchangia kiasi cha shilingi 500.00 kwa siku kama gharama ya usafi na kwa
kipindi cha Julai, 2023 hadi Juni, 2024, soko hili limeweza kukusanya kiasi cha
shilingi milioni 460 katika shilingi bilioni 1 iliyokasimiwa sawa na asilimia
46 ya lengo” alisema Dkt. Sagamiko.
Alisema
kuwa ujenzi wa soko hilo umeliweka Jiji la Dodoma katika mandhari safi na
kurahisisha shughuli za usafi na utunzaji wa mazingira. Ujenzi huo umerahisisha
utoa wa huduma za msingi kwa wafanyabiashara. “Halmashauri ili kuweza kufikia
lengo la bajeti iliyowekwa tayari imeandaa mikakati ifatayo. Tayari halmashauri
iemshatengeneza tenda na imempata mzabuni atakayehusika kukusanya ushuru na
kodi kwa wafanyabiashara wote ndani ya soko. Halmashauri inaendelea na zoezi la
kuelimisha wafanyabiashara kupitia viongozi wao juu ya ulipaji ushuru na
utunzaji wa miondombinu ya soko. Kwa kushirikiana na viongozi wa soko halmshauri
imeadaa kutatua changamoto mbalimbali zinapojitokeza kwa lengo la kuboresha
mazingira ya biashara kwa kundi hili” alisema Dkt. Sagamiko.
Kamati
ya kudumu ya Bunge ya Tamisemi ilifanya ziara ya kawaida ya kutembelea na
kukagua maendeleo ya uendeshaji wa Soko la wazi la Machinga lililojengwa katika
Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa zaidi ya shilingi bilioni tisa likiwa na
uwezo wa kubeba zaidi ya wafanyabiashara 3,000.
MWISHO
Comments
Post a Comment