WASIMAMIZI WA VITUO VYA UCHAGIZI NDOGO WA DIWANI KATA YA NALA WAASWA
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
WASIMAMIZI
wa vituo vya uchaguzi mdogo wa Diwani Kata ya Nala wametakiwa kufanya kazi kwa
nidhami, hekima na uzalendo na kuepuka kuisababishia serikali hasara.
![]() |
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, John Kayombo akiwaapisha wasimamizi wa vituo vya uchaguzi mdogo Kata ya Nala |
Kauli
hiyo ilitolewa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, John Kayombo
alipokuwa akifungua mafunzo kwa wasimamizi wakuu na wasimamizi wasaidizi kwenye
vituo vya uchaguzi mdogo wa Diwani Kata ya Nala, Jimbo la Dodoma mjini
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jiji la Dodoma.
Kayombo
ambae ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema “niwaombe sana
wasimamizi wa vituo, uchaguzi ni suala nyeti sana sikiliza kwa makini maelekezo
ya viongozi na fuata taratibu na sheria zilizopo, ukikosea utaitia serikali
katika hasara kubwa. Kuweni na nidhamu, hekima na uzalendo kwa kiwango cha juu
sana. Baadhi yenu mlishasimamia chaguzi nyingi ila uchaguzi hauhitaji mazoea.
Tusiweke mazoea katika suala la uchaguzi”.
Alisema
kuwa matarajio ni uchaguzi huo kufanyika vizuri na kumalizika salama. “Ninyi
mmeaminika miongoni mwa watanzania wengi. Fanyeni kazi hii kwa uadilifu,
uaminifu mkubwa kwa kushirikiana na wenzenu kama timu moja ili tumalize salama.
Kama unajisikia huwezi kufanya kazi hii tuambie mapema upumzike” alisema
Kayombo.
Kwa
upande wake Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa,
Mhe. Mwanaisha Kwariko aliwapongeza wasimamizi hao kwa kuaminiwa na kuchaguliwa
kati ya wengi walioomba. “Lazima uheshimu hiyo dhamana uliyopewa kwa kufanya
kazi hiyo kwa uaminifu. Niwaase kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo
kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kama kuna jambo limekutatiza uliza” alisema
Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Kwariko.
Aidha,
aliwataka kuheshimu kiapo chao cha kutunza siri na kuwaeleza kuwa kukiuka kiapo
hicho wanaweza kushitakiwa kwa sheria husika. “Msiwe mashabiki wa vyama vya
siasa, mmeshaapa kujitoa kwenye vyama vya siasa. Mnatakiwa kuhudumia watu wote
kwa usawa” alisisitiza Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Kwariko.
Akielezea
sifa za wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa vituo, Mratibu wa Uchaguzi,
Albert Kasoga alisema ni lazima awe raia wa Tanzania mwenye umri wa kuanzia
miaka 18 na kuendelea. Sifa nyingine alizitaja kuwa ni uadilifu na utiifu
mwenye akili timamu. “Hatakiwi kuwa shabiki au kiongozi wa chama chochote cha
siasa. Awe amehitimu elimu ya kidato cha Nne au zaidi na anaweza kusoma na
kuandika vizuri na anaweza kuelewa vizuri maelekezo ya wasimamizi wa vituo vya
kupigia kura” alisema Kasoga.
Uchaguzi
mdogo wa Kata ya Nala unatarajia kufanyika tarehe 19 Septemba, 2023.
MWISHO
Comments
Post a Comment