Waziri Kikwete Ahimiza Uwajibikaji na Ubunifu kwa Watumishi wa Umma

Na. Bupe Mwaiseje - MAELEZO

Watumishi wa umma nchini wamehimizwa kuzingatia uwajibikaji na ubunifu katika kutekeleza majukumu yao ili kuboresha huduma za Serikali zinazotolewa kwa wananchi.

Akizungumza katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete wakati akifungua Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma, amesema kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa umma ili kuwawezesha kutoa huduma bora na zenye ufanisi.

 


Ambapo alitoa wito kwa watumishi wa umma kuiishi kauli mbiu ya mwaka 2026 inayosema “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu” inayolenga kuwakumbusha watumishi hao wa umma kutambua nafasi yao katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma zinazostahili.

“Niwaombe watumishi wa umma wote kuuishi ujumbe huu, kwani uwajibikaji ndio msingi wa uongozi na utumishi wa umma unaozingatia mahitaji ya wananchi,” amesisitiza Mhe. Kikwete

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Juma  Mkomi, amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya utoaji huduma kwa kutumia teknolojia, uwazi na ushirikiano wa taasisi mbalimbali na kuwa maadhimisho hayo ni fursa kwa taasisi za umma kukutana na wananchi, kupokea maoni na mrejesho utakaosaidia kuboresha utoaji wa huduma.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameipongeza Serikali kwa hatua za kuboresha mazingira ya watumishi wa umma, kuongeza ajira na kuimarisha huduma kwa wananchi.

 

 

Comments

Popular Posts

Bodaboda Mtaa wa Kigamboni wanufaika na Kliniki ya kutatua kero

Ujenzi wa madarasa 3 S/M Mazengo kukamilika Julai, 2026