Gari la Darasa Tembezi latembelea Dodoma Media College
Na. Asteria Frank, DODOMA
Gari
la Darasa Tembezi kutoka Halmashauri ya Jiji Dodoma limetembelea Dodoma Media
College kwa lengo la kuelimisha kuhusu uandikishaji wa orodha ya wapiga kura kuelelea
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Gari
la Darasa Tembezi limewapa wanafunzi wa chuo hicho elimu ya kujiandikisha
kwenye orodha wapiga kura zoezi liloanza tarehe 11 Oktoba, 2024 na kuendelea
hadi tarehe 20 Oktoba, 2024 na kuwataka washiriki katika Uchaguzi wa Serikali
za Mitaa kwasababu ni haki yao na ni muhimu kuchagua viongozi wa mitaa
wanayoishi.
Mwenyekiti
wa uelimishaji na uhamasishaji wa Darasa
Tembezi, Shadaiya Hassan aliwaelimisha
wanafunzi kuwa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27
Novemba, 2024 na kusema kuwa wanatakiwa kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga
kura katika ofisi za mitaa, shule za msingi na sekondari, zahanati na vituo vya
afya, maeneo ya wazi yenye mikusanyiko ya watu na majengo mengine ya taasisi za
umma yaliyopo katika mitaa au vitongoji ili aweze kushiriki kuchagua mwenyeki
pamoja na wajumbe wa kamati ya utekelezaji.
Alisema
kuwa kuna utofauti kati ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura
ambalo linamfanya mwananchi kupata kadi ya kupigia kura mwaka 2025 kwenye
kuchagua diwani, mbunge na raisi. Kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura ni
kwaajili ya kupata sifa ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na linabeba orodha
ya wananchi wanaoishi katika eneo husika.
“Zoezi
la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura halihusiani kabisa na Uchaguzi
wa Serikaliza Mitaa. Kwahiyo, ili kupata sifa ya kushiriki Uchaguzi wa Serikari
za Mitaa ni lazima ujiandikishe kwenye orodha ya wapiga kura katika mitaa
tunayotoka” alisema Hassan.
Aliongeza
kuwa kupata sifa ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni lazima uwe Raia
wa Tanzania, uwe na umri wa miaka 18 na kuendelea , ni mkazi wa mtaa ambao
uchaguzi unafanyika, uwe na akili timamu na awe amejiandikisha kupigakura
katika mitaa husika na zoezi la kujiandikisha ni la mda mfupi.
Mwanafuzi
wa ngazi ya Cheti wa Dodoma Media College, Martin Tulo alisema kuwa Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa unatuhusu watu wote tofauti na dhana aliyokuwa nayo kuwa wagombea
wa uchaguzi ni watu wenye umri mkubwa na wazee kumbe na vijana tunapaswa
kushiriki sio tu kupiga kura hata kugombea.
“Kama
vijana kuna faida nyingi za kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikiwa moja
wapo ni kupata haki yako ya msingi, kushiriki katika vikao vya maamuzi na pia
kupata uzoefu wa uongozi kwa wale wanaotaka kuja kuwa wanasiasa hapo mbeleni”
alisema Tulo.
MWISHO
Comments
Post a Comment