Wafanyabiashara Dodoma washauriwa kujiandikisha orodha ya wapiga kura
Na.
Faraja Mbise, DODOMA
Wafanyabiashara
wameshauriwa kutumia haki yao ya msingi ya kikatiba kupiga kura kwa
kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura ili waweze kupiga kura na kuwachagua
viongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Meneja wa Kidia Vision Hotel, William Moshi
Ushauri
huo ulitolewa na Meneja wa Kidia Vision Hotel, William Moshi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
kuhusu umuhimu wa wafanyabiashara kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura
ili kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa nje ya hoteli yake.
Moshi ambae ni moja ya wafanyabiashara maarufu alisema kuwa anawahamasisha wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kujitokeza
kushiriki zoezi la kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura. Kupiga kura ni
haki ya msingi ya kikatiba. Wananchi watumie fursa hiyo kuchagua viongozi wa Serikali
za Mitaa ili kuepukana na madhara yote yatakayojitokeza pindi wasipojiandikisha
katika orodha ya wapiga kura na kushindwa kuwachagua viongozi bora.
“Nawasihi
wakazi wote na wafanyabiashara wa Jiji la Dodoma na wakazi wengine wote,
kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha kutumia haki yao ya msingi ya kikatiba, kuchagua
viongozi wao kwa ajili ya maendeleo yao na ya taifa. Hakuna mtu mwingine anayeweza
kukuchagulia wewe kiongozi anaefaa bali ni wewe mwenyewe mkazi wa mtaa katika Halmashauri
ya Jiji la Dodoma. Wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla tujitokeze kwa wingi
tukajiandikishe kwenye orodha ya wapiga kura” alisema Moshi.
Akiongelea
uchaguzi wa viongozi bora, alisema kuwa wanachaguliwa na watu wenyewe kwa ajili
ya maendeleo yao. “Hakuna mtu mwingine mwenye wajibu wa kukuchagulia kiongozi,
bali ni wewe mfanyabiashara, mwananchi na mkazi wa kawaida kutumia nafasi hii
ya kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura ili uweze kuchagua kiongozi
anaekufaa kwa ajili ya maendeleo yako na taifa lako” alisisitiza Moshi.
Akiongelea
madhara ya mtu kupoteza sifa ya kuwa mpiga kura katika uchaguzi wa serikali za
mitaa alisema kuwa ni kutojiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura. “Madhara ambayo
yanatokana na kutojitokeza kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura, kwanza,
hutoweza kupiga kura na kama hutoweza kupiga kura utakuwa umepoteza haki yako
ya msingi ndani ya miaka mitano ya kumchagua kiongozi ambaye unaona anafaa. Madhara
mengine utabaki unalalamika kuwa kiongozi ambaye yupo madarakani hafai, wakati
ulipewa nafasi hukuitumia. Halmashauri ya Jiji la Dodoma takribani wiki mbili,
tatu inatangaza kwenye magari ya matangazo wananchi wajitokeze kujiandikisha”
alisisitiza Moshi.
Pia
aliwashauri wananchi wenye sifa na vigezo vya kupiga kura na kuandikishwa
kwenye orodha ya wapiga kura wajitokeze kwa wingi kabla zoezi halijaisha ili
waweze kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua na kuchaguliwa katika Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa. “Mpiga kura anapaswa awe ametimiza umri wa mika 18 na
kundelea, anatakiwa awe na akili timamu ili aweze kutambua ni kiongozi gani
anayeweza na kufaa kumuongoza, kiongozi gani anaweza kufaa kuwa chachu ya
maendeleo katika nchi hii, awe mkazi wa mtaa husika, awe amejiandikisha katika
orodha ya wapiga kura katika mtaa husika na awe ni raia wa Tanzania. ‘Serikali
za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi’
MWISHO
Comments
Post a Comment