MIL. 544,335,626 ZAJENGA SHULE YA SEKONDARI MICHESE

Na. Dennis Gondwe, MKONZE

SHILINGI 544,335,626 zimekamilisha ujenzi wa Shule ya Sekondari Michese na kuwawezesha wanafunzi 555 kupata elimu ya sekondari karibu na maeneo wanayoishi na kuwaondolea kero ya kutembea umbari mrefu kufuata elimu.



Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alipokuwa akisoma taarifa ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Michese kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI iliyotembelea na kukagua ujenzi wa shule hiyo.

Fungo alisema “kiasi cha fedha kilichotolewa kwa ajili ya ujenzi ni shilingi 544,225,626 chanzo cha fedha kikiwa ni SEQUIP. Fedha zilipokelewa Mwezi Oktoba, 2023 na ujenzi ulianza rasmi Mwezi Novemba, 2023 na kukamilika Mwezi Mei, mwaka 2024. Utaratibu wa ujenzi uliotumika ni force akaunti na mradi ulikamilíka kwa wakati na shule ilianza rasmi mwaka 2024 na kusajiliwa kwa jina la Michese Sekondari, Namba ya usajili S.6625”.

Alisema kuwa ujenzi wa shule hiyo ulifanyika kwa awamu tatu, awamu ya kwanza ilihusisha ujenzi wa shule yenye vyumba nane vya madarasa, maabara tatu, maktaba moja, jengo la TEHAMA moja, jengo la utawala moja na matundu 10 ya vyoo.

Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji ilitoa shilingi 20,000,000 ikiwa ni mapato ya ndani kwa ajili ya uchimbaji wa kisima cha maji safi. “Awamu ya pili ya ujenzi ilihusisha ujenzi wa nyumba ya mwalimu, jumla ya Shilingi 95,000,000 ilitolewa Mwezi Juni, 2024 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu 2 in 1. Chanzo cha fedha ikiwa ni SEQUIP. Ujenzi ulianza Mwezi Septemba, 2024 na kukamilika Mwezi Januari, 2025 na kwa sasa nyumba hiyo inatumika” alisema Fungo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, Florent Kyombo akimshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu na kuwawezesha wanafunzi kusoma karibu na maeneo wanayoishi.

Shule ya Sekondari Michese ni shule mpya ya kutwa yenye jumla ya wanafunzi 555 na walimu 30, ilianzishwa Julai 1, 2024 na ipo Kata ya Mkonze, Mtaa wa Michese Bwawani.

MWISHO

 

Comments

Popular Posts

JIJI LA DODOMA LATOA VIWANJA 1,900 KWA WAFANYAKAZI

Ofisi ya Kata Zuzu yaboreshwa kwaajili ya utoaji huduma bora