Mtakwimu Mdoya mbabe Mchezo wa Drafti
Na. Shahanazi Subeti, DODOMA Mtakwimu wa Jiji la Dodoma, William Mdoya ameibuka mshindi katika Mchezo wa Drafti baada ya kumfunga Afisa Michezo, Peter Ititi kwa jumla ya mabao 2-1 ambapo mchezo huo ulilazimika kwenda kwenye muda wa ziada baada ya muda wa kawaida kufungana bao 1-1. Baada ya ushindi huo alisema “ nafurahia ushindi kwa sababu ndio kitu nilichokuwa nakitarajia katika bonanza hili, mchezo ulikuwa mzuri, wachezaji wote niliokutana nao walikuwa wazuri na walionesha ushindani ndiyo maana katika mchezo wa fainali tulienda hadi muda wa ziada ” alisema Mdoya. Nae, Mwalimu Stephen Sebastian, ambaye ni mmoja wa washiriki wa mchezo wa Drafti amekiri kushindwa, hii ni kutokana na ubora wa mpinzani wake. “ Mpinzani wangu alikuwa ni mzuri na anaonekana ni mzoefu katika kucheza drafti na katika mchezo ninakiri kwamba, kuna kushindwa na kushinda na nakubali mpinzani wangu amenizidi mbinu na ujanja katika mchezo huu ” alisema Sebastian. Kwa upande wake Mwamuzi wa Mchezo wa Drafti,...

Comments
Post a Comment