Ujenzi Ofisi Kata Mbalawala watakiwa kukamilika kwa wakati

Na. Leah Mabalwe, MBALAWALA

Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Mbalawala watakiwa kukamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma kwa urahisi.





Hayo yalizungumzwa na Mhandisi wa Jiji la Dodoma, Mhandisi Ally Bella, katika zoezi la ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyofanywa na Kamati ya Fedha na Utawala robo ya tatu 2024/2025 katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Alisema “ninakuagiza Afisa Mtendaji wa kata hii ya Mbalawala kusimamia mradi huu uweze kukamilika kwa haraka kwasababu wananchi wa eneo hili wanategemea ofisi hii kwaajili ya kupata huduma” alisema Mhandisi Bella.

Nae, Awadhi Abdallah, Diwani wa Kata ya Zuzu aliishukuru Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kazi nzuri ambayo inaendelea kuifanya katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo. “Binafsi niishukuru Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo, kwasababu kazi za maendeleo zinaendelea kufanyika katika kila maeneno na sehemu ambazo hakuna basi Jiji la Dodoma linafika katika eneo hilo na kufanya shughuli za maendeleo ikiwa ni ujenzi wa shule, barabara pamoja na vituo vya afya. Kwa sasa Dodoma ni Jiji ambalo linafanya maendeleo ya hali ya juu pasipo na miradi ya serikali kuu, halmashauri inapeleka miradi ili wananchi waweze kunufaika nayo” alisema Abdallah.


Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Mbalawala umegharimu kiasi cha shilingi 20,000,000, fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

MWISHO

Comments

Popular Posts

Agenda ya Lishe yaongeza Ari ya usomaji S/M Dodoma Makulu

Miaka minne ya Dkt. Samia, Kizota yanufaika mikopo ya asilimia 10

Halmashauri ya Jiji la Dodoma Kuhudumia Majimbo Mawili ya Uchaguzi