Waziri Mkuu Mstaafu, Pinda atembelea NSSF, Maonesho ya Nanenane Dodoma
Na. Mwandishi wetu, DODOMA
Waziri
Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda ametembelea
Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na
Ofisi hiyo pamoja na Taasisi zake ikiwemo NSSF. Maonesho ya Nanenane 2025
Kitaifa yanaendelea katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma ambapo kilele chake
ni tarehe 8 Agosti 2025.
Akitoa maelezo mbele ya Mhe. Pinda, Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Yahya Mudhihir, alieleza namna ambavyo NSSF imeboresha utoaji wa huduma kwa kutumia mifumo ya kidijitali, hatua inayolenga kuongeza ufanisi, uwazi na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanachama na wadau.
Alisema
kuwa mwanachama anaweza kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na NSSF bila
kulazimika kufika ofisini, ikiwemo, usajili wa wanachama wapya kupitia mfumo ya
kidijitali, uwasilishaji na ukusanyaji wa michango ya waajiri na wanachama na
kulipa mafao mbalimbali.
Aliongeza
kuwa NSSF inashiriki maonesho haya kwa lengo la kutoa elimu ya hifadhi ya jamii
ikiwemo elimu kuhusu mafao, jinsi ya kujisajili wanachama wapya kutoka sekta
binafsi na wananchi waliojiajiri, elimu kuhusu kujichangia kupitia simu ya
kiganganjani popote walipo, pia kutangaza fursa za uwekezaji katika miradi ya
nyumba na viwanja, elimu kuhusu huduma za Mifumo mbalimbali ikiwemo Lango la
Huduma (NSSF Portal) pamoja na elimu ya mapambano dhidi ya Rushwa.
Aidha,
alimweleza Waziri Mkuu Mstaafu kuwa NSSF katika kutanua wigo wake wa uwekezaji,
umewekeza katika mradi wa kimkakati ambao ni Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi
ambacho ni ubia na Jeshi la Magereza.
Kwa
upande wake Mhe. Pinda alisema kuwa Kiwanda cha Sukari Mkulazi ni ushahidi wa namna
taasisi za Serikali zinavyoweza kuwekeza katika miradi yenye tija kwa taifa
hasa kwa kutumia rasilimali zao ili kuboresha maisha ya Watanzania, kukuza
uchumi wa taifa na kuleta mapinduzi ya viwanda.
Comments
Post a Comment