Bustani inayohamishika mbombozi kwa wenye maeneo haba ya Kilimo

Na. Mwandishi wetu, DODOMA

Mafunzo yanayotolewa katika vyuo vya VETA yanalenga kuleta utatuzi wa changamoto mbalimbali katika jamii.




Watu wengi wanaoishi katika maeneo ya mijini wamekuwa na maeneo finyu kwa ajili ya kilimo, hali hiyo ikampelekea Mwl. Gema Ngoo wa Chuo cha VETA Kihonda, kubuni bustani ya mbogamboga inayohamishika.

Akizungumza katika Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo (Nanenane), yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma Mwl. Ngoo ambaye anafundisha Fani ya Ufundi wa Zana za Kilimo alisema ubunifu huo wa bustani inayohamishika ni mahkususi kwa wale watu wanaoishi katika nyumba za kupanga, nyumba zenye maeneo finyu au zilizosakafiwa kote, hivyo kupelekea kukosa sehemu ya kupanda mbogamboga.

“Ubunifu huu utawasaidia wengi wenye maeneo finyu kwaajili ya kupanda mbogamboga, tunashauri watu walime kilimo cha aina hii kwani hakiharibu mazingira lakinini pia kilimo hiki utatumia mbolea ya asili ambayo ni salama kwa afya za binadamu” alisema Mwl. Ngoo.




Mwalimu Gema aliwaalika wananchi wa Dodoma na mikoa jirani kutembelea banda la VETA lililopo katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma ili kujifunza ubunifu na kupata taarifa za fursa za mafunzo mbalimbali katika vyuo vya VETA.

 

Comments

Popular Posts

Jiji la Dodoma lapewa angalizo lishe bora kwa wananchi

RC Dodoma apongeza wafugaji kwa ushiriki wa Paredi ya Mifugo

Vijana waalikwa kushiriki Kongamano S/M Mbwanga