Manaibu Makatibu Wakuu OR TAMISEMI Watembelea Banda la TARURA
Na. Mwandishi wetu, DODOMA
Manaibu
Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI wakiongozwa na Mhandisi Rogatus
Mativila Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu), Sospeter Mtwale - Naibu Katibu
Mkuu (TAMISEMI) na Prof. Tumaini Nagu - Naibu Katibu Mkuu (Afya) wametembea
Banda la Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika kilele cha
Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima NaneNane katika Viwanja vya Nzuguni, jijini
Dodoma.
Makatibu Wakuu hao walipatiwa maelezo mbalimbali kutoka kwa wataalamu wa TARURA wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Catherine Sungura kuhusu majukumu, utekelezaji wa miradi mbalimbali pamoja na mipango ya TARURA inayohusu uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya barabara nchini.
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake Naibu Katibu Mkuu, Sospeter Mtwale amewapongeza TARURA kwa
kazi nzuri wanayoifanya ya kufungua barabara hususan maeneo ya wakulima, wavuvi
na wafugaji na hivyo kuwarahisishia kusafirisha mazao yao.
Pia
alisema barabara hizo zimesaidia waendesha bodaboda na waendesha vyombo vya
moto vingine na hivyo kupata ajira hivyo kuwataka kuendelea kuboresha barabara
za vijijini ili ziweze kupitika wakati wote.
Comments
Post a Comment