Pinda ataka matokeo ya Utafiti yazingatiwe kueleza faidia za Kisanyansi katika bidhaa za Kilimo

Na. Mwandishi wetu, DODOMA

Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda ametaka Utaalamu wa Kisanyansi uzingatiwe katika mnyororo mzima wa thamani wa sekta ya Kilimo ikiwa ni pamoja na kuzingatia ufafanuzi wa Kisanyansi katika chapa za bidhaa mbalimbali za Kilimo zilizoongezewa thamani ili kuonesha tija inayopatikana kwa mtumiaji wa bidhaa hizo.



Mhe. Pinda alisema hayo alipotembelea Banda la Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kwenye Maonesho ya kimataifa ya Kilimo maarufu kama Nanenane yanayoendelea viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma ambapo TARI inashiriki ikiwa na Teknolojia mbalimbali za Kilimo.

Akitolea mfano wa Korosho iliyoongezewa thamani na TARI Mhe. Pinda alieleza kufuraishwa na ufafanuzi wa kitaalamu uliopo katika mfuko wa Korosho hizo unaotoa maelezo ya Kisanyansi kumtosheleza mtumiaji kutambua tija anayopata kutokana na matumizi ya bidhaa hiyo zaidi ya kuishia kusema ni tamu yenye ladha nzuri kitu ambacho amesema kinanyima fursa zaidi kwa mtumiaji kuelewa.
Akiwa katika Banda la TARI, Waziri Mkuu huyo mstaafu alipata maelezo kuhusu Teknolojia mbalimbali za Kilimo zilizofanyiwa Utafiti na TARI ambazo amewasihi wadau wa Kilimo kuzitumia ili kujiongezea tija.

 




 

Comments

Popular Posts

Jiji la Dodoma lapewa angalizo lishe bora kwa wananchi

RC Dodoma apongeza wafugaji kwa ushiriki wa Paredi ya Mifugo

Vijana waalikwa kushiriki Kongamano S/M Mbwanga