Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu yafungua Masoko ya Nje kwa Wafanyabiashara nchini
Na. Calvin Gwabara, DODOMA
Mamlaka
ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imewezesha Tanzania kuondolewa
vikwazo vya kiubora iliyowekewa kwenye masoko mbalimbali duniani na hivyo
kusaidia wakulima wa Tanzania kunufaika na uuzaji wa mazao nje ya nchi.
Hayo yalibainishwa na mtaalamu wa afya ya mimea kutoka TPHPA, Dorah Amur wakati akimueleza Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alipotembela banda la TPHPA kwenye maonesho ya wakulima Nanenane kitaifa Jijini Dodoma kuhusu mafanikio na jitihada zinazofanywa na Taasisi hiyo katika kuhakikisha ubora wa mazao na kufungua masoko.
“Wakulima wa wafanya biashara wa Tanzania wamekuwa wakiuza bidhaa zao kwenye
masoko mbalimbali ya kimataifa duniani lakini kuna baadhi ya masoko yalizuia
Tanzania kuingiza bidhaa zetu kutokana na sababu mbalimbali za kiubora lakini
TPHPA ikaalifanyia kazi haraka kwa kufanya uchunguzi wa kina na kuwasilisha
kwenye mamlaka za masoko hayo na kufanikiwa kuondolewa kwa zuio hilo na sasa
Tanzania inauza bidhaa hzo bila shida” alifafanua Amuli.
Hata hivyo mtaalamu huyo amesema pamoja na masoko ya mbali lakini pia nchi
inanufaika na kuuza mazao kwenye masoko ya afrika mashariki kwani takwimu
zinaonesha Tanzania imesafirisha zaidi zao la mchele kwenda kwenye nchi hizo
kwa wingi hasa nchini Uganda, ikifuatiwa na Kenya, Rwanda na DRC katika kipindi
cha kuanzia mwaka 2024 hadi mwezi Mei mwaka 2025.
“Mamla ya Afya ya mimea na viuatilifu Tanzania inajivunia kusaidia wakulima na wafanyabishara wa Tanzania kuyafikia masoko mbalimbali lakini pia kusaidia kuwezesha nchi kunufaika na mauzo ya bidhaa hizo kwa kuhakikisha ubora wa bidhaa zinazosafirishwa na zile zinazoingia kukidhi viwango vya ubora” alieleza Bi. Amuli.
Akizungumzia masuala ya ufungashaji wa bidhaa zinazosafirishwa meneja wa usimamizi wa Afya ya Mimea na karantini kutoka TPHPA, Musa Chindinda alisema kuwa hilo ni eneo muhimu ambalo taasisi hiyo inalizingatia na kuhakikisha bidhaa zinazosafirishwa zinakuwa katika hali ya ubora na salama.
“Sio tuu kwamba tunaangalia ubora wa zile zinazosafirishwa lakini pia tunashirikiana na mamlaka zingine kupima na kuhakikisha hata bidhaa zinazoingia nchini zinazingatia ubora hususani vyakula ili kuepusha kuingiza mazao au bidhaa zenye vidudu au magonjwa hatari ambayo yanaweza pelekea kuwekwa kwa karantini” alieleza Chidinda.
Pia alimueleza Balozi hatua mbalimbali ambazo zinapaswa kuzingatiwa ili kupata kibali kinachoweza kuruhusu bidhaa hizo kupokelewa na pia kutoa ushauri kwa wafanyabiashara wanaotaka kuuza bidhaa nje ya Tanzania.
Kwa upande wake Balozi huyo wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alipongeza juhudi hizo kubwa zinazofanywa na TPHPA katika kusaidia kufungua masoko ya bidhaa za Tanzania duniani na kuahidi kuendelea kushirikiana na katika masoko mbalimbali ya mazao nchini Italia.
“Nimefurahi kuona Italia pia bidhaa za Tanzania zinavyopata masoko duniani na kuinua uchumi wa watu na kuingiza nchi fedha za kigeni, Hii sio kazi ndogo hasa kusaidia kuondoa mashaka yanaywekwa na masoko kwa bidhaa za Tanzania kwakweli mnastahili pongezi na niwaombe muendelee kusaidia nchi yetu nami kama balozi nipo tayari kushirikiana nanyi kwenye mambo yoyote ya kimasoko nchini Italia alieleza Mhe. Balozi Mbarouk.
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania inashiriki maonesho ya Kilimo Nanenane kitaifa jijini Dodoma na kwenye Kanda zote kupitia ofisi za kanda za Mamlaka hiyo kote nchini.
Comments
Post a Comment