VETA yapongezwa kutoa mafunzo kwa wanawake na Samia
Na. Mwandishi wetu, DODOMA
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imepongezwa kwa
kuendelea kutoa mafunzo ya ufundi stadi kupitia
Mpango wa mafunzo unaotekelezwa na Taasisi ya Wanawake na Samia.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ambae ndie muasisi wa Taasisi hiyo, alipotembelea banda la VETA lililopo katika viwanja vya Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo (Nanenane), Nzuguni, jijini Dodoma na kuongea na wahitimu wa mafunzo hayo wanaoonesha bidhaa mbalimbali walizotengeneza baada ya kupata mafunzo kutika vyuo vya VETA.
“Tunafahamu fika kwamba Mhe. Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akihimiza
utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi kwa makundi maalum wakiwepo wanawake.
Naipongeza VETA kwa kuendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa kuwa tunaona matokeo
yake kupitia bidhaa na bunifu mbalimbali zinazofanywa na wanawake hapa Dodoma
na kote nchini” alisema Senyamule.
VETA imeendelea kutoa mafunzo ya aina mbalimbali kwa Taasisi ya Wanawake
na Samia kupitia vyuo vyake kote nchini.
Comments
Post a Comment