Mtaji Benki ya TADB wafikia Bil. 442
Na. Mwandishi wetu, DODOMA
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imemshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza katika uwezeshaji
wakulima kwa kuwapatia mikopo ya Pembejeo.
Akitoa maelezo kwa Mhe. Rais Samia kuhusu utendaji wa Benki hiyo leo Agosti 8,2025 wakati wa maadhimisho ya kilele cha Nanenane kitaifa, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Frank Nyabundege alisema kuwa mtaji wa Benki hiyo umekuwa kutoka shilingi bilioni 60 hadi bilioni 442.
“Benki yetu itaendelea kudhamini maonesho ya NnNe Nane kwa kipindi cha miaka
mitano mfululizo kwa sababu imeiwezesha kuwa na mtaji mkubwa” alisisitiza
Nyabundege.
Mgeni rasmi katika maonesho ya Nanenane Kitaifa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Comments
Post a Comment