Mtendaji Mkuu WMA atembelea Maonesho ya Nanenane Dodoma
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla,
leo Agosti 8, 2025 ametembelea Maonesho ya Nanenane kitaifa, katika uwanja wa
Nzuguni jijini Dodoma.
Akiwa katika Banda la WMA, Afisa Mtendaji Mkuu aliwapongeza watumishi wa Wakala kwa kazi nzuri ya kuelimisha umma ambayo wamekuwa wakiifanya tangu kuanza kwa Maonesho hayo.
Aliwataka kuendelea kutoa elimu ya vipimo kwa jamii hata
baada ya Maonesho ili wananchi waelewe ni kwa namna gani Serikali kupitia WMA
inawalinda kwa kuhakikisha vipimo vinavyotumika katika sekta mbalimbali ni
sahihi na vinatumika kwa usahihi. “Tuendelee kutumia majukwaa mbalimbali
kutoa elimu ya vipimo kwa wananchi ili waelewe haki yao ya kupata huduma kwa
vipimo sahihi lakini pia na wajibu wao wa kuhakikisha wanatumia vipimo sahihi
katika sekta mbalimbali” alisema Kihulla.
Vilevile, alitembelea mabanda mengine mbalimbali likiwemo
banda la Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Taasisi zake ili kujionea
huduma zinazotolewa.
Comments
Post a Comment