Uwanja wa Maonesho wa Nanenane wafurika
Na. Flora Nadoo, NANENANE
Uwanja wa maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati
Dodoma, wafurika watu kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya kushuhudia ufunguzi
huo.
Mbali na ufunguzi huo wa maonesho ya Nanenane,
wananchi washuhudia uzinduzi wa Tukutuku (Pikipiki za miguu mitatu) takribani
100 ambazo zitagawiwa kwa vijana. Kupitia pikipiki hizo vijana watapata faida
kubwa sana kwasababu ni pikipiki zilizotengenezwa kisasa zaidi na hivyo
zitakuwa zinatoa kahawa ya viwango vya juu sana.
Kwa upande wa burudani, wananchi walifurahia sana
wagogo wakicheza ngoma zao za asili kwa umahili mkubwa wakiongozwa na mwalimu
wao aliyefahamika kwa jina la Malima.
Kutokana na kufurika kwa
watu hao, watu wenye vyombo vya moto kama bajaji, pikipiki na magari wajipatia
faida kubwa tofauti na siku zote kufuatia kutoa huduma ya usafiri.
Habari hii imehaririwa
na Janeth Gerald
MWISHO
Comments
Post a Comment