Bodaboda Mtaa wa Kigamboni wanufaika na Kliniki ya kutatua kero

Na. Mwandishi wetu, KIKUYU KASKAZINI

MTAA wa Kigamboni umewatembelea maafisa usafirishaji kusikiliza changamoto zao na kuwaelezea fursa ya mikopo isiyo na riba ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ili waweze kunufaika nayo.



Akizungumza na maafisa usafirishaji wa Mtaa wa Kigamboni Kata ya Kikuyu Kaskazini, Afisa Mtendaji Mtaa wa Kigamboni, Farijala Kunga alisema kuwa serikali ina wajibu wa kuwatembelea na kuwasikiliza wananchi wake.

“Leo Serikali ya Mtaa wa Kigamboni imewatembelea maafisa usafirishaji (waendesha bodaboda) katika Mtaa wa Kigamboni kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi. Huu ni utekelezaji wa maelekezo ya serikali wa kuyafikia makundi mbalimbali kuyasikiliza na kutatua kero zao. Aidha, tumewaelezea fursa za mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri ya jiji la Dodoma kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Tumewapa elimu kuhusu manufaa ya kiuchumi ya mikopo hiyo ukiwa ni mkakati wa serikali ya awamu ya sita wa kuwawezesha wananchi wake kiuchumi” alisema Kunga.

Ziara hiyo ni muendelezo wa kliniki ya siku tatu ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi iliyoanza tarehe 11-13 Juni, 2026 ikitoa huduma za upimaji wa afya, msaada wa kisheria, huduma za kifedha kutoka benki ya NMB, RITA, TRA na NSSF.


MWISHO

Comments

Popular Posts

Ujenzi wa madarasa 3 S/M Mazengo kukamilika Julai, 2026