Katambi: Vijana watakiwa kuyajua mema ya serikali

Na. Mwandishi wetu, DODOMA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amewataka vijana wa Wilaya ya Dodoma kuyajua mema ya serikali ambayo ina neema kwa kila kijana nchini kuanzia aliyesoma hata ambae hajasoma.


Akizungumza leo katika Kongamono la Vijana kuelekea mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 wenye Kaulimbiu isemayo ‘Tanzania ni yetu sote tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo’, lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini.

“Amini haujazaliwa kwa bahati mbaya, bali kwa kusudi la Mungu uliamliwa wewe uwe Mtanzania na sio nchi nyingine. Jambo la msingi ni kujitambua na kujua wajibu wako pia kujua wewe una ndoto gani na uzisimamie ndoto zako, na serikari inawajibu wa kuandaa mazingira wezeshi kwenu kwa sababu ni moja ya majukumu yake muhimu. Pia ni sehemu ya nne katika kukutengeneza wewe, Mungu kwanza, wazazi, jamii kisha serikali. Hivyo, fursa ni nyingi kwenu simamieni misimamo yenu na ajira zote ni zenu nyinyi vijana” alisema Katambi.

“Kipekee nimependa maneno ya waziri, hotuba yake imenipa imani mpya kwasababu nilikuwa nasoma kwa kukata tamaa ukiangalia ajira hamna unawaza utaenda wapi. Lakini hapa nimetoka nikiwa na matumaini ya kutosha kabisa fursa ni nyingi kwaajili yangu kikubwa ni kuwajibika ili nitimize malengo yangu” alisema mshiriki wa kongamano hilo Doren Ahimidiwe.



Kwa upande wake James Kimaro alisema aliishukuru serikali kwa kuwakutanisha vijana katika kongamano hilo. “Naishukru serikali kwa kutuletea hii ‘vijana platform’ kwasababu ndio uwanja wa sisi kutoa maoni na kutatuliwa changamoto zetu. Lakini pia kongamano hili limekuja na mada ambazo moja kwa moja sisi vijana ni sehemu yake. Mfano, mada ya uzalendo katika mitandao ya kijamii sisi vijana ndio wahangwa wakubwa wa upotoshaji na upotoshwaji. Hivyo, kipekee elimu nimeipokea na naomba iwe endelevu kwetu” alisema Kimaro.

Ikumbukwe Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 zinatarajiwa kuingia katika Wilaya ya Dodoma tarehe 1 Juni, 2026 na kutembelea miradi saba ya maendeleo.

MWISHO

Comments

Popular Posts

Baraza la Madiwani Jiji la Dodoma lawafukuza kazi watumishi watatu na mmoja kushushwa cheo

Odero: Mwenge wa Uhuru alama ya Umoja Wilayani Dodoma