Kimaro: Wananchi Dodoma waalikwa kuupokea Mwenge wa Uhuru Juni, 1 2026

 

Na. Mwandishi Wetu, DODOMA

Mwenyekiti wa Kamati ya Chakula katika maandalizi ya Mwenge wa Uhuru 2026 Wilaya ya Dodoma, Dickson Kimaro anawaalika wananchi kushiriki mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru na kuwakumbusha kuwa tukio hilo linawaungansha pamoja na kujenga mshikamano wa kimaendeleo.


Mwenyekiti wa Kamati ya huduma ya Chakula Wilaya ya Dodoma

Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma unaotarajiwa kuwasili tarehe 1 Juni, 2026 na kukimbizwa katika miradi saba ya maendeleo.

Alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri. “Maandalizi mpaka leo hii yapo vizuri na Kamati ya Chakula imejipanga katika eneo la chakula kwa kuhakikisha wote wanaohudhuria wanapata chai itakayotolewa katika Shule ya Sekondari, Dkt. Samia na chakula cha mchana kitakuwepo pale katika Shule ya Sekondari Umonga. Chakula cha usiku kitapatikana katika shule ya Msingi Kizota’’ alisema Kimaro.

Kimaro ambae pia ni Mkuu wa Kitengo cha Usafi na udhibiti wa taka ngumu Jiji la Dodoma alisema kuwa kitengo kipo tayari  kuupokea Mwenge wa Uhuru 2026 na kutoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi kuupokea na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru katika miradi yote wilayani Dodoma.

Mwenge wa Uhuru 2026 utawasili katika Wilaya ya Dodoma tarehe 1 Juni, 2026 ukiongozwa na kaulimbiu isemayo ’’Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo’’.

MWISHO

Comments

Popular Posts

Baraza la Madiwani Jiji la Dodoma lawafukuza kazi watumishi watatu na mmoja kushushwa cheo

Odero: Mwenge wa Uhuru alama ya Umoja Wilayani Dodoma

Mwenge wa Uhuru waridhishwa na ujenzi wa Barabara yenye urefu wa KM 1.6 kiwango cha lami