Jiji la Dodoma lakusanya 104% Mapato ya ndani 2024/2025
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
HALMASHAURI
ya Jiji la Dodoma ilikusanya shilingi 65,042,215,034 sawa na asilimia 104 ya
lengo la mwaka la mapato ya ndani kwa Mwaka wa Fedha 2024/ 2025.
Kauli
hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick
Sagamiko alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha
kuanzia Mwezi Juni hadi Oktoba, 2025 katika mkutano wa kwanza wa halmashauri
baada ya uchaguzi mkuu wa Rais, Watunge na Madiwani.
Alisema
kuwa baada ya kuvunjwa kwa Baraza la Madiwani Mwaka 2025/2026 Menejimenti ya
Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliendelea na jukumu la kukamilisha ukusanyaji wa
mapato kwa kipindi cha mwaka 2024/2025. “Kwa Mwaka huo wa fedha, halmashauri
ilikusudia kukusanya shilingi 143,164,202,949.46 na hadi kufikia tarehe 30
Juni, 2025, ukusanyaji wa mapato ya ndani ulikuwa shilingi 65,042,215,034 sawa
na asilimia 104 ya lengo la mwaka na kufanya ukusanyaji wa mapato yote ya
halmashauri kuwa shilingi 152,269,204,654 sawa na asilimia 106” alisema Dkt.
Sagamiko.
Alisema
kuwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 halmashauri iliidhinishiwa kukusanya na kupokea
jumla ya shilingi 164,579,966,999.99 ikiwa ni mapato yatokanayo na vyanzo vya
ndani, ruzuku ya mishahara, ruzuku ya matumizi mengineyo na fedha kwa ajili ya
miradi ya maendeleo. “Kwa kipindi cha Julai hadi Oktoba, 2025, jumla ya
shilingi 22,193,124,132.17 zimekusanywa sawa na asilimia 30.96 ya lengo la
makisio ya mwaka” alisema Dkt. Sagamiko.
Wakati
huohuo, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri aliwataka madiwani kusimamia ukusanyaji wa
mapato ya halmashauri. “Mstahiki Meya, nendeni mkasimamie halmashauri yetu
iendelee kuwa mahili katika kukusanya mapato, mmepewa taarifa hapa kwamba
asilimia 104 ya mapato imekusanywa na kuvuka lengo la mwaka ulioisha.
MWISHO
Comments
Post a Comment