Mstahiki Meya Chaula ashauri Baraza kutumia mkakati wa hoja kwa hoja

Na. Mwandishi Wetu, DODOMA

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Alimwoni Chaula ameshauri Baraza la Madiwani kujenga utaratibu wa kuwasilisha hoja moja na kuiazimia hadi itakapokamilika ndio hoja nyingine ifanyiwe kazi.



Aliyazungumza hayo kwa msisitizo katika mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri jijini Dodoma.

Alisema kuwa mkakati huo wa hoja moja ‘Focus Strategy’ ndiyo njia pekee ya kuleta maendeleo yanayoonekana na yenye tija kwa wananchi wanaowaongoza. "Ili tuwe na ufanisi, niwaombe kwa unyenyekevu mkubwa sana tuchague jambo moja na kuliazimia hadi mwisho. Kwa mfano, kama baraza linaona kipaumbele ni ujenzi wa matundu ya vyoo kwa shule zote za msingi katika jiji letu, basi nguvu, fedha, na usimamizi wetu wote uelekezwe hapo. Tukimaliza na kujiridhisha kuwa kila shule ina vyoo bora, ndipo tunahamia hoja nyingine ya msingi na kuendelea na mtiririko huo" alisema Chaula.

Alimalizia kwa kutoa rai kuwa umoja na maamuzi ya pamoja yatawasaidia kuwa kitu kimoja na kwamba washirikiane kuhakikisha shughuli za kimaendeleo za Jiji la Dodoma zinafaniwa.








MWISHO

Comments

Popular Posts

Juhudi na nidhamu yatakiwa kwa washiriki wa mafunzo ya Jeshi la Akiba Dodoma

Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshiriki kongamano la Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma kwa siku mbili likiwa na lengo la kukumbushana majukumu ya kazi, kupitia sera mpya zilizoandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na kutoka na mpango kazi mpya wa kutekeleza katika maeneo yao ya kazi.