Timu ya ‘sustainability’ ya Jiji la Dodoma yaanza semina ya siku saba
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA
Mafunzo maalum kuhusu viwango vipya vya uhasibu
‘General
Requirements for Disclosure of Sustainability-related Financial Information na Climate-related
Disclosures’ (IFRS S1 na IFRS S2) yameanza rasmi kutolewa kwa timu ya
‘sustainability’ ikiwa ni sehemu ya mpango wa mafunzo ya uendelevu
‘sustainabilty and ESG’ yanayolenga kuwajengea uelewa na kuongeza ufanisi
katika usimamizi wa taarifa za kifedha.
Akizungumza wakati wa semina hiyo ya siku ya kwanza, Mratibu wa Mafunzo ya ‘sustainability’ katika Jiji la Dodoma, Akida Huddu alisema kuwa mafunzo hayo yamelenga kutoa elimu ya jumla ya uendelevu ‘sustainability and ESG’ kwa washiriki ili kuwawezesha kusimamia kwa ufanisi shughuli zote zinazohusiana na uendelevu pamoja na kupata taarifa zitakazosaidia kutoa huduma nzuri kwa wananchi.
Aliongeza kuwa uelewa wa viwango vipya vya uhasibu ni
muhimu katika kuimarisha uwazi, uwajibikaji na usimamizi bora wa rasilimali za
umma, hususan katika mazingira yanayohitaji uendelevu wa taasisi. “Timu hii
itashiriki mafunzo ya siku saba na leo ndio tumeanza. Mafunzo haya yanatolewa
kwa lengo la kufuata taratatibu za viwango vipya vya mahesabu IFRS S1 na IFRS S2. Ni imani yetu kuwa hadi
mwisho wa mafunzo washiriki watakuwa wamepata elimu ya kutosha itakayoleta
manufaa katika kutimiza mpango huu” aliongeza Huddu.
Kwa upande wake, Afisa TEHAMA wa Jiji la Dodoma, Eva Shafraeli alipongeza mafunzo hayo na kusema kuwa yana umuhimu mkubwa katika kusaidia utoaji mzuri wa huduma kwa wananchi. “Mafunzo haya yanatufundisha kufanya uendelevu bila kusababisha athari kubwa kwa mfano kutunza mazingira. Haya yote tuliyojifunza leo ni mafunzo mazuri na yatatusaidia kufanya kazi katika mazingira rafiki na kutoa huduma nzuri kwa wananchi” alipongeza Shafraeli.
Nae, Afisa Elimu Maalum wa Jiji la Dodoma, Mwl. Issa
Kambi alisema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kusimamia uendelevu wa masuala
yote yaliyoanzishwa na halmashauri ili yasonge mbele na kuleta matokeo chanya
yasiyo na athari. “Kwa mfano katika mazingira kuhakikisha masuala mazima ya
mazingira yanasimamiwa vizuri, miti inapandwa ili kuondoa vihatarishi kama
mafuriko, ukame, uchafuzi wa mazingira na uchafuzi wa hali ya hewa ambavyo kwa ujumla
visipoangaliwa vinaweza kuturudisha nyuma katika masuala ya ukuaji wa uchumi
wetu” alisema Mwl. Kambi.
Kwa ujumla ‘sustainability team’ inapaswa kusimamia
uendelevu kwa kuzingatia kizazi kijacho ili nacho kije kikutane na masuala
muhimu yaliyoanzishwa yenye lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora
na rafiki.
MWISHO
Comments
Post a Comment