Wanafunzi wa ‘field’ wapelekwe kwenye kata
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof.
Davis Mwamfupe amewataka wanafunzi wanaofanya mafunzo kwa vitendo katika Halmashauri
ya Jiji la Dodoma kwenda kwenye kata kufanya kazi za jamii ili kupata uzoefu
tofauti.
Kauli hiyo aliitoa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani
wa kuwasilisha taarifa za utekelezaji kutoka kwenye kata uliyofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa halmashauri.
Prof. Mwamfupe alisema “idadi ya wanafunzi wa ‘field’
ni kubwa, waende kwenye kata kufanya kazi za jamii. Wapo waandishi wa habari hapa,
habari hazipo kwa Mstahiki Meya na Mkurugenzi pekee, waende kwenye kata. Hii itawanufaisha
wao kwa kupata uzoefu na kutakuwa na mafuriko ya habari zinazohusu kata na
maendeleo ya wananchi”.
Kwa upande wake Flora Nadoo alisema kuwa kauli ya Mshahiki
Meya ni nzuri kwa sababu wanavyoenda kwenye kata wanajifunza vitu vingi na
kujua changamoto zinazowakabili wananchi moja kwa moja. “Vile unavyoenda kuona
kwa macho na kuja kuandika habari inakuwa na uzito kuliko unapoandika kutoka
kwa mzungumzaji” alisema Nadoo.
Nae Emmanuel Lucas alisema kuwa kitendo cha waandishi
wa habari wanaojifunza kutoka ofisi kuu ya jiji kwenda kufanya kazi za habari kwenye
kata na kuziwasilisha kwa wasimamizi wa halmashauri ni jambo zuri. “Kwa sababu
halipo nje ya malengo ya ‘field’ ya kujifunza na kupata uzoefu mbalimbali” Lucas.
Kwa upande wa mwanafunzi wa ‘field’ ya uandshi wa habari,
Moureen John alisema “nakubaliana na Mstahiki Meya kwa sababu huko kwenye kata
kuna matukio mengi yanayoendelea na sisi hatuyafahamu. Hivyo, tukienda kwenye
kata tutapata matukio mengi ya habari za kuwafahamisha wananchi”.
MWISHO
Comments
Post a Comment