Baraza la Madiwani Dodoma lampongeza Rais fedha za miradi
Na. John Masanja, KATA YA VIWANDANI
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya
Jiji la Dodoma lampongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuhakikisha serikali
inapeleka fedha za kutosha katika maendeleo na kutekeleza ujenzi wa miradi
mbalimbali nchini hususani ndani ya Jiji la Dodoma.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe |
Hayo yalisemwa na Mstahiki Meya wa
Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe wakati akifungua Mkutano wa Baraza la
Madiwani kwa ajili ya kuwasilisha taarifa za utekelezaji kutoka kwenye kata,
uliofanyinya katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
“Hakuna ubishi wowote kuhusu jinsi
serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ilivyopoleka pesa
kwa ajili ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya nchi, hili halina ubishi”
alisema Prof. Mwamfupe.
Aidha, Pro. Mwamfupe aliwata wajumbe
wa mkutano huo kuendelea kutoa ujumbe na elimu kwa wananchi kuhusu jitihada za
Serikali ya Awamu ya Sita katika kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo pamoja na
uboreshwaji wa huduma, zinavyoleta manufaa kwa jamii na kuzitazama fursa
mbalimbali zilizopo kwenye ujio wa miradi hiyo.
“Twendeni zaidi kwa wananchi wetu wa
kawaida na kuwaeleza, wazitumieje fursa hizo zilizopo kwenye ujio wa miradi
mbalimbali kama huu wa Treni ya Mwendokasi (SGR)” aliongeza Prof. Mwamfupe.
Akizungumza mara baada ya
uwasilishwaji wa taarifa hizo, Daudi Mkhandi, Diwani wa Kata ya Nkuhungu,
aliipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa
miradi na kusema kuwa imesaidia kupunguza kadhia mbalimbali kwa wananchi huku
akishauri kumaliziwa kwa miradi viporo katika mwaka mpya wa fedha 2024/25.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya
Kilimani, Neema Mwaluko alisema kwa mara ya kwanza ndani ya mwaka wa fedha
2023/24, Kata ya Kilimani imefanikiwa kujegewa Shule mpya ya Msingi ya kwanza
ya Chinyoya na kusema kuwa kupitia uwepo wa shule hiyo utakwenda kupunguza
changamoto ya umbali kwa wananfunzi waliokuwa wakienda kusoma katika maeneo ya
mbali na wanapoishi.
MWISHO
Comments
Post a Comment