Madiwani Jiji la Dodoma washauriwa kushirikiana na wadau wa maendeleo
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo
amewashauri madiwani kujenga uhusiano mzuri na wadau wa maendeleo waliopo
katika kata ili wasaidie kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mkurugenzi wa Jiji, John Kayombo akifafanua jambo
Kayombo alitoa kauli hiyo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani
wa kuwasilisha taarifa za utekelezaji kutoka kwenye kata uliyofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa halmashauri.
Kayombo alisema “wadau wa maendeleo kwenye kata wapo
wengi tuwatumie ili kuunga mkono utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata”.
MWISHO
Comments
Post a Comment