Mbunge Mavunde akabidhi Kompyuta kwa Kata 41 za Jiji la Dodoma
Na. Nancy Kivuyo, VIWANDANI Watendaji wa Kata 41 za Halmashauri ya Jiji la Dodoma wapokea Kompyuta na Printa kwa ajili ya kurahisisha na kuboresha utendaji kazi wenye ufanisi za kuwahudumia wananchi. Vifaa hivyo, viligawiwa katika hafla ya Ugawaji Kompyuta na Printa kwa Shule za Sekondari za Serikali na Watendaji wa Kata jijini Dodoma, iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Viwandani. Akizungumza wakati wa ugawaji kompyuta hizo, Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde, alisema kuwa anawapa kompyuta maafisa watendaji wa kata zote 41 kwaajili ya kuwasaidia kufanya kazi zao kidigitali zaidi. “Kompyuta na printa hizi natumaini zitachochea utendaji kazi ulio mzuri. Tuipongeze serikali chini ya uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maboresho makubwa ya miundombinu kwenye sekta ya elimu jijini Dodoma ambapo kwa mwaka huu wa fedha zimetengwa shilingi bilioni 16” alisema Mavunde. Nae, Afisa Mtendaji wa Kata ya Hazina, Tunu Mahmoud, alisema kuwa ameguswa na tukio l...
Comments
Post a Comment