JIJI LA DODOMA LATOA VIWANJA MBADALA 1,105 KWA WANANCHI
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
HALMASHAURI
ya Jiji la Dodoma imetoa viwanja mbadala 1,105 kwa wananchi katika kutekeleza
mkakati wake wa kumaliza migogoro ya Ardhi jijini hapa.
![]() |
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, John Kayombo akongea na waandishi wa habari |
Kauli
hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Kliniki ya
Ardhi iliyo katika siku yake ya pili ya kutatua migogoro ya Ardhi jijini hapa.
Kayombo
alisema kuwa wakati anafika Dodoma kulikuwa na wananchi takribani 4,000
wanaodai viwanja mbadala. “Yaani kiwanja kimoja kimegawiwa kwa mwananchi zaidi
ya mmoja. Lakini mpaka sasa tumeshatoa viwanja 1,105 kufidia wale wananchi.
Mpaka sasa tunadaiwa viwanja 2,895. Matarajio mpaka kufikia mwezi Desemba mwaka
huu tutakiwa tumekamilisha kutoa viwanja hivyo 2,895. Kwa sababu kuna zoezi
kubwa linaendelea la kupima eneo la Mahomanyika viwanja vitapatikana 7,000 na
tutaoa viwanja 2,895 na kuwapatia wananchi viwanja vyao” alisema Kayombo.
Kliniki
ya Ardhi imewaweka pamoja wataalam wote wa sekta ya Ardhi ili kupokea, kusikiliza
na kutatua migogoro ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
MWISHO
Comments
Post a Comment