JIJI LA DODOMA LATAMBUA JITIHADA ZA MWANAMKE WA KIJIJINI
Na. Dennis Gondwe, CHIHANGA
HALMASHAURI
ya Jiji la Dodoma inatambua jitihada zinazofanywa na mwanamke wa kijijini
katika uzalishaji wa chakula na kusimamia lishe ya familia.
Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii, Charity Sichona |
Kauli
hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Jiji
la Dodoma, Charity Sichona alipokuwa akiongea maadhimisho ya siku ya mwanamke
anayeishi kijijini ofisini kwake leo ambayo yatafanyika katika Kata ya Chihanga
jijini Dodoma.
Sichona
alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaadhimisha siku hiyo kwa lengo la
kuendelea kutambua jitihada za mwanamke anayeishi kijijini. “Wanawake wanaoishi
vijijini wanamchango mkubwa katika kuzalisha chakula na kuchangia uwepo wa
chakula katika familia na nchi nzima. Hivyo, serikali imeamua kutambua jitihada
zao za kilimo, ufugaji na shughuli za kiuchumi na kuwatia moyo ili waendelee
kuzalisha wakati serikali ikiendelea kutatua changamoto zinawakabili” alisema
Sichona.
Sichona
alisema kuwa mwanamke wa kijijini anapowezeshwa kufanya shughuli zake bila
vikwazo familia, halmashauri na taifa kwa ujumla litakuwa na uhakika wa chakula
na hadi kuwa na chakula cha akiba. “Mwanamke ni mtendaji mzuri katika kazi za
uzalishaji. Hii siku inatambua zile jitihada zinazofanywa na mwanamke huyu ili
kuzipa thamani” aliongeza.
Akiongelea
baadhi ya program zinazowezeshwa na serikali alisema kuwa zipo kwa ajili ya
kuwasaidia wanawake kukua kiuchumi. “Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewezesha
program mbalimbali. Mfano Kizazi cha Usawa, hii inatambua jitihada za wanawake
wanazofanya na wanapewa elimu juu ya uzalishaji, masuala ya kilimo, mifugo na kazi
za mikono ili kuendeleza uchumi wao na kuleta usawa katika kumiliki mali na
ardhi ili mwanamke awe na usawa katika masuala ya kiuchumi” alisema Sichona.
Kwan
upande wake mkazi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Hadija Sued alisema kuwa ni
mara yake ya kwanza kusikia maadhimisho hayo. Alisema kuwa maadhimisho hayo ni
muhimu kwa sababu yatawahamasisha wanawake kuongeza juhudi katika shughuli zao
za uzalishaji mali.
Maadhimisho
ya Siku ya mwanamke anayeishi kijijini mwaka 2023 yaliongozwa na kaulimbiu
isemayo “Wezesha wanawake vijijini kwa uhakika wa chakula; lishe na uendelevu
wa chakula”.
MWISHO
Comments
Post a Comment