Na. Dennis Gondwe, KIWANJA CHA NDEGE WANANCHI wa Mtaa wa Osterbay, Kata ya Kiwanja cha Ndege Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamejitokeza kufanya usafi wa mazingira katika eneo la Shule ya Msingi Mlimwa B kwa lengo la kuweka mazingira safi na kuepuka na magonjwa ya mlipuko kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla. Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mtendaji Mtaa wa Osterbay, Ashura Iberia alipokuwa akiongea na wananchi wa Mtaa wa Osterbay waliojitokeza kwa wingi kufanya usafi wa mazingira katika Shule ya Msingi Mlimwa B. Iberia alisema “leo tumefanya usafi wa mazingira kuzunguka Shule ya Msingi Mlimwa B, wananchi wa Mtaa wa Osterbay wamejitokeza kwa wingi kufanya usafi wa mazingira. Lengo la kufanya usafi huo ni kuweka mazingira ya shule safi ili wanafunzi ambao ni watoto wetu wasome katika mazingira safi na salama. Lakini pia kuwaepusha wanafunzi na jamii inayozunguka shule hii na magonjwa ya mlipuko. Zoezi hili nimelisimamia mimi mwenyewe Afisa Mtendaji Mtaa wa Osterbay ili kutoa cha...
Comments
Post a Comment