Mkurugenzi wa Jiji awatakia Heri ya Mwaka Mpya 2025 Wafanyakazi
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt.
Frederick Sagamiko amewatakia heri ya mwaka mpya 2025 wafanyakazi wote katika Bonanza
kubwa michezo katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Akifungua bonanza hilo lililoandaliwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa ajili ya kuwakutanisha wafanyakazi na kuuaga mwaka 2024 na kuukaribisha mwaka 2025, Mkurugenzi wa Jiji alisema kuwa michezo inalenga kuwakutanisha wafanyakazi na kuwakumbusha kuwa ni wamoja na wanatakiwa kufanya kazi kwa upendo na kushirikiana.
Akiongelea umuhimu wa michezo katika kujenga urafiki
na umoja alisema kuwa hilo halina mjadala. “Karibu sana katika uwanja wa Jamhuri.
Tumekutana hapa taasisi zaidi ya moja katika uwanja huu lakini wote lengo letu
ni moja la michezo kwa afya zetu. Ushauri wangu Dodoma Jiji wenye ratiba wakutane
na Ofisi ya Rais, Ikulu ‘kuharmonise’ ratiba ili tuona tutakavyoshirikiano pamoja.
Heri ya Mwaka mpya 2025” alisema Dkt. Sagamiko.
Kwa upande wake Mwl. Sylvia Madeje kutoka shule ya
Sekondari Chinangali alimpongeza mkurugenzi wa jiji na timu yake kwa kuandaa
bonanza hilo kubwa la michezo kwa wafanyakazi. “Michezo inadumisha ushirikiano
kwa wafanyakazi, kuongeza ufanisi kwa sababu pamoja na michezo tunabadilishana
mawazo na kuimarisha ari ya utendaji wa kazi” alisema Madeje.
Bonanza kubwa la michezo la wafanyakazi wa Halmashauri
ya Jiji la Dodoma lilitanguliwa na mbio za polepole (jogging) zilizoanzia Ofisi
kuu ya Jiji zikiongozwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuelekea uwanja wa
michezo wa Jamhuri kuanzia saa 12.30 alfajiri.
=30=
Comments
Post a Comment