Kamba wanaume Ofisi ya Rais Ikulu yaiburuza kwa taabu Ofisi ya Rais Jiji la Dodoma
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
Timu ya Kuvuta Kamba wanaume kutoka Ofisi ya Rais
Ikulu imeiburuza kwa taabu sana Timu ya Kuvuta Kamba wanaume ya Ofisi ya Rais
Jiji la Dodoma kwa mivuto miwili mtawalia katika Bonanza la michezo.
Katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini
hapa, timu zote zilionesha kukamiana kutokana na kuwa chini ya mwavuli mmoja ambao
ni Ofisi ya Rais.
Aidha, mwamuzi wa mchezo huo alilazimika mara kadhaa kutumia
filimbi yake kuzikumbusha timu zote mbili kanuni za mchezo huo wa kiuvuta kamba.
Mchazo ulianza kwa nguvu na kila upande ulionesha unaweza ibuka mshindi.
Ofisi ya Rais Ikulu iliibuka kidedea kwa kuiburuza kwa
taabu sana Ofisi ya Rais Jiji la Dodoma kwa mivuto miwili bila majibu.
Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliandaa Bonanza la
michezo mbalimbali la wafanyakazi kwa lengo la kuwakutanisha na kufurahia kuuaga
mwaka 2024 na kuukaribisha mwaka 2025 katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
MWISHO
Comments
Post a Comment