RC Senyamule apokea Bendera ya Taifa kutoka Mkoa wa Kigoma Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Na. Faraja Mbise, DODOMA


MIAKA 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara yavuka mikoa katika Jiji la Dodoma baada ya Muendesha Baiskeli kutoka Mkoa wa Kigoma, Wenseslaus Lugaya kuendesha baiskeli hadi Mkoa wa Dodoma ikiwa ni ushiriki wake katika Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo tarehe 9 Desemba, 2024. 

Akiwa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Lugaya alimkabidhi Bendera ya Taifa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule tukio lililoshuhudiwa na mamia ya wakazi wa Jiji la Dodoma wakiongozwa na mkuu wa mkoa. Viongozi wengine walioshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Fungo na maafisa waandamizi wa serikali na sekta binafsi.


Matukio ya picha za zoezi husika


Muendesha Baiskeli kutoka Mkoa wa Kigoma, Wenseslaus Lugaya (wa pili kulia) akitoa maelezo ya utangulizi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule (wa pili kushoto)




Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akitoa tabasamu la miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara baada ya kupokea Bendera ya Taifa kutoka kwa Muendesha Baiskeli kutoka Mkoa wa Kigoma, Wenseslaus Lugaya


Comments

Popular Posts

Osterbay Dodoma wajitokeza usafi wa mazingira

Usafi wa Mazingira Kipaumbele Kata ya Chamwino

Wananchi wa Kata ya Mtumba wanufaika na Mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri