Sepesha Rushwa, Acha Rushwa ya Ngono
Na. Coletha Charles, DODOMA
Mkuu
wa Wilaya ya Kongwa, Mayeka Simion Mayeka ametoa wito kwa vijana wa Wilaya ya
Dodoma kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kujihusisha na
kampeni mbalimbali za kuleta tija na mabadiliko katika nchi kwa sababu ni nguzo
ya taifa na mchango muhimu katika kufanikisha ndoto za maendeleo.
Mayeka
alisema hayo wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Mgeni Rasmi, Patrobas Katambi, Naibu
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) kwenye kilele cha mbio
ndefu na fupi za Taasisi ya Anti-Corruption Voices Foundation yenye kauli mbiu
ya Badili tabia Shepesha Rushwa katika
shule ya msingi makole.
Alisema
kuwa kupitia mbio hizo wamepeleka ujumbe kwa jamii kama nguzo ya maendeleo na
kutoa pongezi kwa Ant-Corruption Voices Foundation kwa juhudi za kuimalisha
maadili na uwajibikaji kwa sababu ni mfano bora kwa taasisi zisizo za
kiserikali kwa kushirikiana na Serikali kuimalisha maendeleo ya jamii. “Mbio za
Sepesha Rushwa Marathon ni mfano wa ubunifu na jinsi michezo inaweza kuwa
jukwaa la kuhamasisha jamii kuhusu maadili, uwazi na uwajibikaji, tukio hili
siyotu linanatufundisha umuhimu wa kuzingatia afya zetu, bali linatufundisha mshikamano
wa kitaifa zidi ya changamoto zinazotukabili, mbio hizi zinaweza kuwa chachu ya
mabadiliko chanya na kuibua mijadala mbalimbali muhimu kama mapambano zidi ya
rushwa ya ngono na kuhamasisha uwajibikaji katika sekta zote za maisha” alisema
Mayeka.
Mayeka
aliongeza kwa kusema kuwa Tanzania imeshika nafasi ya Pili Ukanda wa Afrika
Mashariki katika mapambano ya Rushwa ikitanguliwa na nchi ya Rwanda, “Ripoti
mbalimbali zinaonyesha rushwa ya ngono ni changamoto kwa wanawake na vijana
madhara ya rushwa ya ngono kazini ni pamoja na kutoa ajira kwa wanawake, kupandishwa cheo, nyongeza za
mishahara, kupewa siku za kupumzika na wanawake wengi wanafanya rushwa ya ngono
kwa kutishiwa kupoteza kazi zao, madhara mengine ya rushwa ya ngono ni
kuchochea maambukizi ya VVU na UKIMWI na inafanyika katika mazingira yasiyo
salama na kuongeza magonjwa ya zinaa” alisema.
Naye,
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri alisema wananchi wanalo jukumu
la kuzuia na kukemea rushwa ya ngono, mapambano zidi ya madawa ya kulevya
Ukimwi na mmonyoko wa maadili kwa vitendo kulingana na maslahi ya Taifa na ukubwa
wa tatizo hili katika jamii kuongezeka hasa kwa vijana na wanawake. “Viongozi Anti-Corruption
Voices Foundation ninawahakikishia ushirikiano na ulezi, tumewapatia ofisi tunawawezesha
kwa vitu mbalimbali, kadili tulivyo jaliwa na mwenyezi mungu tuendelee kuwaunga
mkono lakini pia kuwaunganisha na wadau wengine ili kusudi mapambano haya dhidi
ya rushwa yaweze kuleta matokea katika nchi yetu, ofisi ya mkuu wa wilaya na
wadau wengine tutaendelea kutoa msukumo katika mapambano haya, mnafahamu sisi tunamipango
mingi ya kupambana na rushwa tuna midahalo ya wanafunzi na wanavyuo pia
tunazungumzia na UKIMWI, mmonyoko wa maadili na mapambano dhidi ya madawa ya
kulevya” alisema Alhaj Shekimweri.
Kwa
upande wake, Balozi wa kupinga Rushwa Shule za Msingi anayesoma Darasa la Nne,
Genesnai Katawa, alisema kuwa rushwa inamuumiza kila mtu ambapo tumekimbia
katika mbio za Sepesha Rushwa Marathon kuwahamasisha wananchi kutojihusisha na
rushwa kwa kufanya mambo yasiyo ya haki. “Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu
Hassan anahakikisha Tanzania inakuwa nchi yenye haki na usawa, kila mtu
anapinga rushwa kwa nguvu sana pia anatufundisha kuwa waaminifu na kufanya kazi
kwa bidii na lakini pia tuungane kama Taifa, tukimbie kwa matumaini katika haki na kuna baadhi ya madhala ya
rushwa katika nchi yetu ni Pamoja na watu kukosa haki zao, kuhamasisha uhalifu
ili kupambana ni kuhamasisha taasisi mbalimbali zina kemea’’ alisema Katawa.
Sepesha
Rushwa Marathon ni Kauli mbiu ya Taasisi ya Ant-Corruption Voices Foundation
yenye ujumbe wa Acha Rushwa ya Ngono, imekuwa ikifanya mbio hizi kwa mda wa
miaka mitatu tangu 2022, kwa lengo la kupinga rushwa ya ngono kazini, shuleni
na vyuoni.
MWISHO
Comments
Post a Comment