Mbunge Mavunde awakumbuka mama lishe Dodoma
Na. Faraja Mbise, DODOMA
Mbunge
wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde, ameahidi kuwatengenezea mazingira
mazuri na rafiki ya kufanyia biashara mama lishe waliopo pembezoni mwa
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Mavunde
alizungumza hayo mara baada ya kumaliza zoezi la uzinduzi wa ujenzi wa jengo la
kupumzikia wananchi lilipo nje ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Aidha,
Mavunde aliahidi kuwaboreshea na kuwatengenezea mazingira rafiki ya kufanya
biashara ya chakula na kukarabati miundombinu kama vile kuwatengenezea meza na
viti za kufanyia biashara pamoja na kuweka maeneo nadhifu.
Mavunde
alisema “sambamba na hilo nafahamu ya kwamba, asilimia kubwa ya wanaokaa pale
hawavimudu vyakula ambavyo watu wengi hapa tunavimudu vyakula vya mahotelini...”.
Hata
hivyo, Mavunde aligusia wananchi wa kipato cha chini wasioweza kumudu gharama
kubwa za kununua chakula kwa ajili ya wagonjwa wao hivyo kuahidi kuwasaidia
mama lishe kuboresha maeneo yao ya kufanyia kazi kuwa safi na salama ili waweze
kutoa huduma nzuri ya chakula kwa wananchi.
Kwa
upande wa mama lishe nao hawakuwa nyuma walipongeza juhudi zinazofanywa na
Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, hususani katika uzinduzi wa ujenzi wa jengo la
kupumzikia wananchi uliofanyika leo hii jijini Dodoma.
Mama
lishe, Pili Elius katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na mkazi wa
Chinyoya alisema “tunamshukuru mbunge wetu kwa alichotufanyia, sisi kama mama
lishe tunamuomba Mungu ampe maisha marefu na hili jengo linalojengwa litaleta
manufaa kwa wanaouguza wagonjwa wao. Miaka mingi sana wanalala hapo nje, mvua
zinawanyeshea na baridi, tunaona ni jambo jema sana kuhusu ujenzi huu”.
Mbunge
wa Jimbo la Dodoma mjini alitoa ahadi hiyo alipokuwa akiongea na mamia ya
wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa ujenzi wa jengo la kupumzikia wananchi
wanaoenda kuona wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kutokana
na changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa mahali pa kupumzikia.
MWISHO
Comments
Post a Comment