Kata ya Chamwino yatekeleza agizo la RC la usafi wa Mazingira
KATA ya Chamwino imetekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule la kufanya usafi kila jumamosi kwa lengo la kuliweka Jiji la Dodoma safi.
Akiongelea utekelezaji wa agizo hilo, Afisa Mtendaji Kata ya Chamwino, Lucas Nkelege alisema kuwa usafi huo ulifanyika katika maeneo ya korongo la Mailimbili na Mwaja. Usafi huo ulihusisha kufyeka vichaka na nyasi, kuokota makopo na mifuko ya plastiki iliyozagaa katika korongo na kuzibua mitaro ya maji yenye urefu wa mita 100, aliongeza.
Alisema
kuwa kata yake ilitumia zoezi hilo la usafi wa pamoja kuwahimiza wananchi
kufanya usafi wa mazingira katika maeneo ya biashara na makazi pamoja na
kuhakikisha wanatunza mazingira katika msimu huu wa sikukuu.
Usafi
wa pamoja katika Kata ya Chamwino ulishirikisha Afisa Mtendaji Kata, Wenyeviti
wa mitaa, mabalozi na wananchi.
Comments
Post a Comment