UJENZI WA NYUMBA YA WALIMU SHULE YA MTEMI CHILOLOMA MSAADA KWA WALIMU
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MRADI
wa ujenzi wa nyumba ya walimu (mbili kwa moja) katika shule ya Sekondari Mtemi
Chiloloma utawasaidia walimu kukaa mazingira ya shule jambo litakaloongeza
ufanisi katika utendaji kazi wao na kutoa matokeo chanya.
Kauli
hiyo ilitolewa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtemi Chiloloma, Mwl. Livinus Tanganyika
alipokuwa akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba ya walimu
(two in one) katika Shule ya Sekondari Mtemi Chiloloma iliyopo Kata ya Hombolo
Makulu Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Mwl.
Tanganyika alisema kuwa serikali kupitia mradi wa kuboresha shule za sekondari
(SEQUIP) ilitoa jumla ya shilingi 95,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya
walimu ambapo lilikuwa ni hitaji kubwa kwa sababu eneo la shule liko mbali na
eneo la makazi ya watu. Fedha za ujenzi ziliingizwa katika akaunti ya shule
tarehe 20/6/2023 na kuvuka mwaka na kuanza kutumika katika mwaka wa fedha
2023/2024.
Akiongelea
utekelezaji wa mradi huo alisema kuwa ulianza tarehe 9 Septemba, 2023 baada ya
taratibu za manunuzi kukamilika na ujenzi unatekelezwa kupitia ‘force account’.
“Mradi huu unahusisha
ujenzi wa nyumba moja ya walimu (two in one) yenye vyumba vitatu, sebule, jiko
na stoo kwa kila nyumba. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 99 ikiwa
bado milango michache ambayo ipo kwa fundi katika hatua ya umaliziaji pamoja na
ufungaji wa vyoo viwili vya kukaa. Mradi unategemea kukamilika kabla au ifikapo
tarehe 25 Novemba, 2023 tayari kwa matumizi” alisema Mwl. Tanganyika.
Kuhusu faida za mradi ukikamilika, alizitaja kuwa
ni walimu kukaa kwenye mazingira ya shule na hivyo kuongeza ufanisi katika
utendaji kazi. Nyingine ni kuwezesha mazingira mazuri ya kuishi kwa walimu,
aliongeza.
“Uongozi wa Shule ya Sekondari Mtemi Chiloloma
unapenda kutoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha hizi
ambazo zinaenda kuboresha maisha ya walimu. Pia tunatoa shukrani kwa Mheshimiwa
Mkuu wa Mkoa, Mheshimiwa Mbunge, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya, Kamati ya Siasa ya
Wilaya kwa maelekezo na usimamizi wa karibu wa miradi yote inayotekelezwa
katika Jiji la Dodoma. Hii yote ni katika kuhakikisha kwamba Ilani ya Chama Cha
Mapinduzi inatekelezwa kwa vitendo” alisema Mwl. Tanganyika.
Ikumbukwe kuwa ujenzi wa Shule ya Shule ya
Sekondari Mtemi Chiloloma umetumia kiasi cha shilingi milioni tisini na nne
laki nane na elfu ishirini na tatu (94,823,000.00) hadi wakati kamati ya Siasa
ya Mkoa wa Dodoma kuitembelea.
MWISHO
Comments
Post a Comment